Monday, April 6, 2015

Monday, April 06, 2015


Afrika Kusini imekuwa na fukwe za utupu ambazo sio rasmi kwa miongo kadhaa. Lakini hii ni mara ya kwanza kwa nchi hiyo kuupata rasmi. Ufukwe wa Mpenjati uliopo kwenye Bahari ya Hindi sasa ni rasmi kutumika hivyo. Kumekuwepo na mapingamizi awali toka kwa wanamazingira na wahifadhi wa uhalisi wa bahari toka mwaka 2014 baada ya Serikali ya Mtaa kutoa idhini ya awali kwa hatua hiyo.



Fukwe za Cape Town, maarufu kama sandy bay, zimekuwa zikitumika kwa namna hiyo kwa miongo kadhaa, japokuwa hazijaidhishwa rasmi.

Mpenjati Beach,iko kilomita 140(maili 90) kusini ya bandari ya Durban ya Afrika Kusini na imekuwa maarufu kama 'strip-off" kwa miaka 20 sasa.
"Kumwkuwa na wasiwasi kutoka kwa wakazi kwa miongo miwili iliyopita," alisema Serge Pavlovic, Mwenyekiti wa South African National Naturist Association (Sanna).

"Mambo yameendelea kuwa mazuri kwa miaka ya hivi sasa, na ni vyema kuwa tumeendelea kueleweka kwamba fukwe za utupu ni jambo la kawaida. Matokeo yamekuwa ni kuufanya rasmi ili tuweze kuja hapa tena na tena, na hakuna haja ya kuogopa kukamatwa sasa," aliiambia AFP.

Pavlovic alisema shughuli zilizopangwa kufanyika  mwishoni mwa wiki itakuwa ni pamoja na mpira wa wavu na gunia.

Hata hivyo, itakuwa vigumu kujenga miundo mbinu katika eneo hio kwani ni ukanda wa bahari ya ulinzi

0 comments: