Sunday, April 12, 2015

Sunday, April 12, 2015




Habari zilizotufikia punde zinasema watu kadhaa ambao idadi yao bado haijafahamika wanasemekana kupoteza maisha baada ya basi la abiria liitwalo Nganga linalofanya safari zake kati ya Iringa na Kilombero kugongana uso kwa uso na lori aina ya Fuso na kisha magari hayo kuteketea kwa moto maeneo ya milimani kilomita kadhaa kutoka Ruaha Mbuyuni kuelekea Morogoro, majira ya saa mbili asubuhi leo. 

Pichani hapa chini ni basi la Nganga wakati na bada ya kuteketea kwa moto. Tunaendelea kufuatilia na tutakuletea taarifa zaidi kadiri zinavyopatikana.

0 comments: