Kiongozi Mkuu wa Chama cha Alliance For Change and Transparency (ACT-Wazalendo) Zitto Kabwe, akiwahutubia wakazi wa mji wa Makambako
mkoani Njombe jana, wakati wa ziara endelevu ya chama hicho
iliyoanzia mikoa ya nyanda za juu kusini.
Rais Jakaya Kikwete ametakiwa kuitisha Bunge Maalum haraka iwezekanavyo ili ili liweze kufanya marekesho madogo ya katika ili kuruhusu uchaguzi ufanyike kwa uhuru na haki.
Kauli hiyo imetolewa na CHAMA cha Alliance For Change and Transparency (ACT-Wazalendo), wakati akizungumza kwa nyakati tofauti Mkoani Njombe na Mji Mdogo wa Makambako wakati wa ziara ya chama hicho ya kuimarisha chama hicho mikoani.
Akizungumza katika mkutano wa hadhara Mwenyekiti wa ACT-Wazalendo, Anna Mghwira, alisema sasa umefika wakati ni lazima nchi iwe huru kwa kuwa na misingi imara itakayoimarisha demokrasia nchini. “Rais aitishe Bunge maalumu ili kufanya marekebisho madogo ya Katiba kuruhusu uchaguzi huru na wa haki lakini pia Wajumbe wa Tume waombe kazi na wawe wataalamu.
“Kwa nini ACT tunashauri kuitwa Bunge Maalumu ni kutokana na uhai wa Bunge la 10 umebakisha mkutano mmoja kabla ya kuvunjwa. “… hivyo Katibu wa Bunge atangaze nafasi za wajumbe wa Tume, kamati ya Bunge ya Katiba Sheria na Utawala itafanya mahojiano ya wazi na kupata majina 22 yatakayopelekwa bungeni,” alisema.
Alisema baada ya kukamilka kwa mchakato huo huo, Bunge litapiga kura kuchagua watu 11 ambao majina yao watapelekwa kwa Rais ambaye naye atawatangaza kuwa makamishna wa Tume huru ya uchaguzi pamoja na kumteua mwenyekiti kutoka miongoni mwa makamishna hao waliopitishwa na Bunge.
Alisema kutokana na hali hiyo ili kuweza kuwa na tume huru ya Uchaguzi, Tanzania inaweza kutumia mfumo uliotumiwa na nchi ya Msumbiji ambayo kila chama kinateua mwakilishi au kufuata utaratibu wa kutangaza majina kupitia Bunge.
“Kama tukifanikiwa kupata tume huru ni wazi mwaka huu tutakuwa na na Uchaguzi huru na haki kuliko miaka yote iliyopita,” alisema
Kwa upande wake Kiongozi wa ACT-Wazalendo, Zitto Kabwe, alisema kuporomoka kwa maadili ya Taifa kutokana na kukosekana na viongozi wanaopinga rushwa kwa vitendo kama ilivyokuwa ikifanywa na Waziri Mkuu wa zamani, Edward Moringe Sokoine.
Kutokana na kukosekana kwa uadilifu kwa viongozi ni wazi sasa Taifa linashindwa kusukumwa na viongozi waliopo Serikalini na badala yake wanaimba uadilifu huku wakishindwa kutekeleza kwa vitendo.
“Kesho nchi inakumbuka kifo cha Sokoine, ambaye alifariki Aprili 12, mwaka 1984 yaani kesho (leo) lakini kifo chake ni wazi kwetu ACT-Wazalendo tunamkumbuka kwa uwajibikaji wake kwa vitendo. “… leo nchi inayumba ufisadi kila kukicha umekuwa ukitamalaki jambo ambalo lilipigwa na Sokoine kwa kuikata rushwa na hata kupinga uhujumu uchumi kwa makusudi nab ado nchi ilisimama katika uadilifu kama tunavyoamini ACT,” alisema.
Alisema kama Sokoine angekuwa hai hakuna kiongozi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), ambaye angetembea barabarani na kufanya wanayofanyika sasa. Azimio la Songea Alisema akiwa Mbunge aliwasilisha hoja mbalimbali ikiwemo utekelezaji wa azimio la Songea ambalo lilitaka uwazi na wajibikaji kwa Serikali.
“Nilipokuwa bungeni nilisema kuwa mikataba yote ni lazima iwe wazi lakini nilikosa kuungwa mkono na wabunge wenzangu na si hilo tu nilisema mishahara ya ya wabunge ikatwe kodi pia sikuungwa mkono je kisa langu ni nini.
“Tulishindwa kutekeleza suala la mikataba ya madini ambapo leo hii wawekezaji wananufaika na madini lakini wananchi wakibaki kuwa watazamaji jambo hili si jema. Nanyi hapa Njombe mna madini mengi mengi kule kwa rafiki yangu Filikunjombe,” alisema Zitto
Alisema si kazi yake kutoa matusi kwani hatua yake ya kuhamia chama kipya cha ACT-Wazalendo, kusiibue malumbano ila waachiwe Watanzania ndio waamuzi wa Leo. "Tumewaletea chama mbacho hamtojutia kwa kuunga mkono kama ikitokea kuwaambia tunakwenda bungeni hatuchukui posho basi hatuchukui kweli kuliko ilivyo sasa,” alisema.
Katibu Mkuu wa Chama cha ACT-Wazalendo, Samson Mwigamba akiwahutubia wakazi wa mji wa Makambako mkoani Njombe jana, wakati wa ziara endelevu ya chama hicho iliyoanzia mikoa ya nyanda za juu Kusini.
Wananchi waliojitokeza kwenye mkutano wa ACT Wazalendo Njombe wakifuatilia kwa makini huku wakinyeshewa na mvua.
Askari wa jeshi la polisi wakiimarisha ulinzi kwenye mkutano wa chama cha ACT-Wazalendo uliofanyika mjini Njombe jana.
0 comments:
Post a Comment