Friday, April 3, 2015

Friday, April 03, 2015


Katika kuadhimisha sikukuu ya Pasaka kwa furaha,wakazi wa jiji la Dar es Salaam na vitongoji vyake wataweza kupata burudani za aina mbalimbali katika tamasha kubwa la Pasaka litakalofanyika katika ufukwe wa Coco beach chini ya maandalizi na udhamini wa kampuni ya simu ya Vodacom Tanzania.

Akiongea juu ya tamasha hili kubwa ambalo hivi sasa limeanza kuwa gumzo ya jiji,Meneja Uhusiano wa Vodacom Tanzania, Matina Nkurlu alisema mipango yote kuhusiana na tamasha hilo imekamilika kinachongojewa ni kuwasha moto wa burudani kwa wateja wa Vodacom na wananchi wote kwa ujumla.

“Kama ilivyo kawaida yetu ya kuwapatia huduma bora wateja wetu sambamba na kuwaburudisha,zamu hii tumewaandalia tamasha hili ili waweze kuburudika katika kuadhimisha sikukuu ya Pasaka na pia watapata fursa ya kukutana na wasanii mbalimbali wawapendao na kuwa karibu nao ukiwa ni mwendelezo wa promosheni ya Vodacom ya kuleta burudani kwa wateja inayojulikana kama Ishi Kistaa”

Meneja huyo alisema kuwa,tamasha hilo litafanyika siku ya Jumapili ya Pasaka na litaanza saa tano asubuhi kwa burudani mbalimbali za muziki na michezo kwa ajili ya watoto kabla ya wasanii mbalimbali wa bongofleva na aina nyingine ya muziki kupanda jukwaani baadaye jioni kutoa burudani kwa washabiki watakaohudhuria tamasha hilo.

Alisema wako wasanii wengi, na wote wamejipanga kutoa burudani ya kutosha kwa wapenzi wa muziki. Kwa uchache aliwataja baadhi yao kuwa ni Shilole,Bob Junior na wengineo. “Wateja na mashabiki watapata fursa ya kuonana na mastaa  ambao wanawapenda pia tunawakumbusha wachukie nafasi ya kushiriki katika promoshe ya Ishi kistaa kwa kutuma neno STAR kwenda 15670”.

Alimalizia kwa kusema kuwa  hali ya amani na usalama inatarajiwa kutawala kwenye tamasha hili kwa kuwa kuna ulinzi wa kutosha kuhakikisha wananchi wanapata burudani murua kwa utulivu,wakiwa na familia zao na akaahidi kuwa wateja wa Vodacom na wananchi wengine wanaokaa mbali na Dar es Salaam wakae mkao wa kula kwani mikakati inaandaliwa kuwapelekea burudani za aina hii katika sehemu mbalimbali nchini kwenye sikukuu mbalimbali zijazo katika siku za usoni.

0 comments: