Friday, April 3, 2015

Friday, April 03, 2015
 JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA NISHATI NA MADINI 
Wizara ya Nishati na Madini (MEM) kwa kushirikiana na Chama cha Wafanyabiashara wa Madini Tanzania (TAMIDA), wanawaalika wadau wote wa Sekta ya Madini na wamiliki wa leseni za biashara ya madini, Masonara na wachimbaji wa madini ya vito kushiriki kwenye Maonesho ya Nne ya Kimataifa ya Vito ya Arusha (Arusha Gem Fair-AGF 2015). Maonesho haya yatafanyika katika hoteli ya Mount Meru ya Arusha, kuanzia tarehe 21 hadi 23 Aprili, 2015.

Maonesho ya AGF kwa mwaka 2015 yanalenga kuendeleza azma ya kuifanya Arusha kuwa kituo cha madini ya vito Afrika. Pia maonesho haya yatawakutanisha washiriki (exhibitors) zaidi ya 100 kutoka nchi za Afrika Mashariki, Kati na Kusini na wanunuzi wa kimataifa zaidi ya 1000 pamoja na wadau mahiri wa tasnia ya vito. Maonesho haya yanadhamiria kuendeleza biashara ya madini ya vito katika nchi za kusini mwa Jangwa la Sahara.

Mabanda ya maonesho yanapatikana kwa gharama za Dola za Marekani 1,000. Kamati ya Maonesho inasimamia ugawaji wa mabanda hayo kwa ushindani (first come-first be served).

Taarifa kuhusu usajili zinapatikana katika Ofisi za Madini za Kanda zilizo katika Miji ya Arusha, Mwanza, Dar es salaam, Mtwara, Mpanda, Shinyanga, Mbeya, Musoma, Songea na Singida au Ofisi za TAMIDA. Wanunuzi wanatakiwa kujisajili kupitia tovuti ya maonesho:www.arushagemshow.com; au kwa barua pepe ya maonesho:info@arushagemshow.com; au kwa njia ya simu zifuatazo 0786366968, 0767498869 na 0767223387.


KATIBU MKUU

0 comments: