Wednesday, April 1, 2015

Wednesday, April 01, 2015
                              
Wakati mgomo wa wafanyabiashara wa kutofungua maduka ukiendelea sehemu mbalimbali nchini,huko mjini Songea mkoani Ruvuma mgomo wa waendesha daladala uliodumu kwa siku nzima jana umesitishwa.



Mwenyekiti wa wasafirishaji wa mkoa wa Ruvuma Bw.Golden Sanga amesema kuwa wameamua kusitisha mgomo wa daladala ili kutoa nafasi ya viongozi kusikiliza malalamiko ya wafanyabiashara huku mgomo wa kutofungua maduka ukiendelea.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa wafanyabiashara mkoa wa Ruvuma Bw.Isaya Mbilinyi amesema kuwa madai yao yasiposikilizwa ya kutatuliwa utata  wa mashine za EFDS,ongezeko la kodi kwa asilimia mia moja na kuachiwa kwa dhamana mwenyekiti wao wa taifa Bw.Johnson Minja mgomo huo utakuwa endelevu.
Kufuatia hali hiyo Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Bw.Said Mwambungu anawasihi wafanyabiashara kusitisha mgomo wao kwa kuwa kuendelea kugoma ni kuwaumiza wasio na hatia bila sababu ya msingi.
Wakati hayo ya kijiri huko tayari Mwenyekiti wa wafanyabiashara Bwana.Johnson Minja amepewa dhamana na Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Dodoma, na baada ya kutekeleza mashati ya dhamana hiyo hivi sasa yuko nje.

0 comments: