Wednesday, May 27, 2015

Wednesday, May 27, 2015

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete akizungumza wakati akifungua rasmi Mkutano wa Nne wa Mabalozi wa Tanzania nje ya nchi. Mkutano huo umefanyika katika Hoteli ya Ramada Jijini Dar es Salaam ukiwa umebeba Kaulimbiu isemayo "Diplomasia ya Tanzania Kuelekea Dira ya Taifa 2025".
Baadhi ya Mabalozi wa Tanzania nchi za nje wakifuatilia hotuba ya ufunguzi ya Mhe. Rais Kikwete (hayupo pichani)
Wajumbe wengine wakiwemo Wakuu wa Vitengo katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wakifutilia hotuba ya Mhe. Rais Kikwete ambaye haonekani pichani.
Rais Kikwete akiendelea na hotuba  ya ufunguzi wa mkutano huo ambapo pamoja na mambo mengine aliwakumbusha Mabalozi  kuwathamini Watanzania waishio nje ya nchi, kuendelea kusaidia upatikanaji wa misaada ya maendeleo, masoko ya bidhaa za Tanzania, wawekezaji na teknolojia bora 
Mhe. Rais Kikwete akimsikiliza Waziri Membe wakati kabla ya kuwahutubia Mabalozi
Mhe. Rais Kikwete akisalimiana na Sekretarieti ya Mkutano wa Nne wa Mabalozi 
Mhe. Rais Kikwete kwa pamoja na Waziri Membe, Naibu Waziri, Mhe. Dkt. Mahadhi Juma Maalim (Mb.), Balozi Sefue,  Balozi Mulamula, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje, Balozi Simba Yahya, Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge, Mhe. Mussa  Zungu, Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Mhe. Paul Makonda wakiwa katika picha ya pamoja na Mabalozi wote .
Mhe. Rais Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na Wakuu wa Idara na Vitengo wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa.

0 comments: