Wednesday, August 19, 2015

Wednesday, August 19, 2015
Wanachama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema katika kata ya Nkoarua Jimbo la Arumeru Mashariki na kata ya Sekei Arusha mjini kwa nyakati tofauti wameandamana kwenye ofisi za chama chao kupinga majina ya wagombea udiwani yaliyopitishwa wakidai kuwepo kwa ukiukwaji wa haki.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti wanachama hao wanasema utaratibu uliotumika  kuwaondoa wagombea walioshinda kwenye kura za maoni unakatisha tamaa na kuonyesha kuwa matakwa ya wengi hayazingatiwi hali inayotishia uhai wa chama.
 
Kwa upande wa wagombea walioshinda na majina yao kukatwa Hagai Kisila wa kata ya Sekei na Samwel Gipson wa kata ya Nkoarua wanasema watafuata taratibu zote kuhakikisha kuwa haki inapatikana.
 
Viongozi wa Chadema wa wilaya ya Arumeru akiwemo Mwenyekiti hawakuwa tayari kuzungumzia sakata hilo kwa kile kilichodaiwa kuwa wana kikao kingine muhimu lakini kwa upande wa Chadema wilaya ya Arusha mbunge wa jimbo hilo Godbless Lema amelazimika kuzungumza kwa niaba ya viongozi ambao hawakuwepo.

0 comments: