Kamati Kuu ya Halmashauri kuu ya Chama cha Mapinduzi imekamilisha kazi ya
uteuzi wa wagombea ubunge katika majimbo mawili ya Singida Mashariki na Kiteto huku ikiteua kamati ya kampeni yenye watu 32 kwa ajili ya
uchaguzi mkuu ujao.
Kamati hiyo itaongozwa na Katibu Mkuu wa chama hicho Bw
Abdulrahiman Kinana. Kwenye majimbo hayo mawili CCM imewapitisha Bw Jonathan Njau kwa jimbo la Singida
Mashariki na Bw Emmanuel John kwa jimbo la Kiteto. Majimbo hayo yamechukuwa
muda mrefu kujadiliwa na kutolewa maamuzi kwa lengo la kupata wagombea
sahihi na wanaokubalika.
Akizungumzia suala la uvumi uliozushwa kwenye mitandao ya kijamii
kuwa ameenguliwa kwenye nafasi hiyo ya ukatibu uenezi na kukabidhiwa Mh
John Chiligati Bw Nape mbali na kulaani uzushi huo amesema wakati huu
ndiyo umuhimu wa sheria ya mitandaoni inaonekana kwani ingekuwa imeanza
kazi kero kama hizo zisingekuwepo.
0 comments:
Post a Comment