Mgombea urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia vyama vinavyounda umoja wa katiba ya wananchi (UKAWA) Mh Edward Lowassa amekamilisha ziara ya kutafuta wadhamini katika visiwa vya Zanzibar na amewaahidi wananchi wa visiwa hivyo kutumia uwezo wake wote kushughulikia kero za muda mrefu zinazowakabili ikiwemo ya muungano, ukiukwaji wa haki za binadamu na wizi wa kura unaofanyika wakati wa uchaguzi.
Akizungumza katika viwanja vya Kibanda Maiti visiwani Zanzibar,Mh Lowassa amesema hatua iliyofikia sasa suala la kuiondoa CCM madarakani halina mjadala kilichobaki ni utekelezaji ambao asilimia kubwa uko mikononi mwa wananchi.
Awali Makamu wa Kwanza wa Rais Mh Seif Sharif Hamad,mgombea mwenza wa Ukawa Mh Duni Haji na Mwenyekiti wa Chadema Mh.Freeman Mbowe kwa pamoja walitumia mkutano huo kuelezea azma ya Ukawa ya kulinda na kudumisha muungano huku pia wakiwataka viongozi wa serikali iliyoko madarakani kuacha kuwatisha watendajihasa wa vyombo vya dola kuwa Ukawa ikiingia madarakani watapoteza ajira zao.
0 comments:
Post a Comment