Monday, August 24, 2015

Monday, August 24, 2015



Umeme wa kutumia gesi asilia unatarajiwa kuanza kutumika mwezi ujao kwa kuunganishwa kwenye gridi ya taifa hadi kituo cha usambazaji cha Tanesco kilicho Kinyerezi,jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na waandishi wa habari kutoka kituo cha kuchakata gesi cha madimba kilicho mkoani Mtwara,Mhandisi Leonce Mroso  amesema, wamefanikiwa kuifungua gesi kutoka kwenye visima na kusafirishwa kwenye kituo hicho kwa ajili ya kuchakatwa.
Amebainisha kuwa gesi hiyo  kwa sasa imekwishachakatwa na inatarajiwa kusafirishwa kwenda Dar es Salaam eneo la kinyerezi  ili kuunganishwa kwenye Gridi ya taifa ifikapo tarehe kumi ya mwezi wa tisa ili iweze kuzalisha umeme.
Hata hivyo amesema gesi hiyo inafaa kutumika majumbani na tayari utafiti umefanyika katika baadhi ya mikoa ikiwemo mkoa wa Dar es Salaam, Mtwara na Lindi.
Kituo hicho kinauwezo wa kuchakata gesi futi za ujazo milioni 80 kwa siku lakini lengo ni kuchakata futi za uchazo milioni 210 kwa siku.

0 comments: