Saturday, August 29, 2015

Saturday, August 29, 2015


Mgombea urais wa Chama cha Mapinduzi Dk. John Pombe Magufuli amewataka watanzania kutofanya maamuzi magumu kama Libya ilivyofanya kwa kumuondoa madarakani rais wa nchi hiyo Muamar Ghadafi na hii leo wamegeuka wakimbizi ndani ya nchi yao.Badala yake, Magufuli amewataka wafanye mabadiliko kama China ilivyofanya katika chama cha Kikomunist cha kufanya mabadiliko ndani ya chama na hivyo na hii leo China imekuwa miongoni mwa nchi za kwanza kiuchumi duniani.

Baada ya ufafanuzi huo kuhusu habari ambazo zimesambazwa katika mitandao ya kijamii Dk.Magufuli ambaye amepewa na wananchi jina la mzee wa kazi akaanza ziara yake ya kusaka ridhaa ya watanzania kiongoza Tanzania mkoani Njombe ambapo amewataka watanzania kupuuza kile kinachoitwa mabadiliko kwa kuwa hata Libya ilifanya mabadiliko ya kukurupuka kutokana na utamu wa lugha za wapinzani wake na hii leo wananchi hao wa Libya wanahangaika na kuwataka kumpa fursa ya urais ili afanye mabadiliko ya kimfumo na kiuchumi taifa lisonge mbele kimaendeleo.

Aidha, mbunge wa Kyela na Waziri wa ushirikiano wa Afrika Mashariki,Dr.Harrison Mwakyembe amewaeleza watanzania kuwa Tanzania haitaki viongozi wa maamuzi magumu na badala yake inamtaka kiongozi mwadilifu atakayesimamia rasilimali za taifa kwa usawa na haki bila uonevu na ambao wanapaswa kuaminiwa na wakipewa madaraka hawatadokoa kwa manufaa yao rasilimali za taifa.

Katokana na kile kinachoneka kuwa sera na kampeni za kistaarabu zinazofanywa na Dr.Magufuli baadhi ya wananchi waliokuwa katika vyama vya upinzani wamerejesha kadi zao na kujiunga na CCM kwa kile walichodai ni kuchoshwa kutumika kama ngazi na viongozi wa Chadema.

Dk.Magufuli anatarajiwa  kuendelea na ziara mkoani Rukwa kesho jumapili Agosti 30.

0 comments: