Saturday, August 29, 2015

Saturday, August 29, 2015
Zaidi ya shahada 30 za kupigia kura katika uchaguzi mkuu utakaofanyika Oktoba 25 mwaka huu zimekamatwa na viongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo ( CHADEMA ) katika kata ya Somanda wilayani Bariadi mkoa wa Simiyu.

Wakizungumzia tukio hilo, watu ambao majina yao yanaonekana kwenye shahada hizo wamelalamikia kitendo cha Tume ya Taifa ya Uchaguzi ( NEC )kushindwa kudhibiti hali hiyo.

Katibu mwenezi wa Chadema Wilaya ya Bariadi, Bw.Martin Morga, ameisea kwamba shahada hizo zimekamatwa katika kata za Somanda na Mhango, ambazo kwa pamoja zipo katika halmashauri ya mji wa bariadi na kuendelea kusema kuwa, suala hilo tayari limefikishwa katika kituo kikuu cha polisi cha Wilaya.

Katika hatua nyingine, Katibu huyo wa Chadema Wilaya amemtaka msimamizi wa uchaguzi jimbo la Bariadi kuingilia kati suala hilo ili kuondoa uwezekano wa shahada hizo kutumika kupiga kura zaidi ya mara moja.

Baadhi ya wakazi wa mji wa Bariadi ambao majina yao yamekutwa kwenye shahada zaidi ya moja,huku wenyewe wakikana kuzitambua wamedai kusikitishwa na hujuma hiyo kwani hali hiyo inaweza kuwatia matatani kwa vile ni kosa kisheria mtu mmoja kujiandikisha zaidi ya mara moja katika daftari la kudumu la wapiga kura

0 comments: