Friday, September 25, 2015

Friday, September 25, 2015
 President Dr. Jakaya Mrisho Kikwete delivers his keynote speech during the 10th  Africa Travel Association  Annual Presidential Forum on Tourism held at New York University Kimmel Center in United States of America this morning.
 Some of the delegates to the 10th ATA Annual Presidential Forum on Tourism held at New York University Kimmel Center in United States of America this morning.
 President Dr.Jakaya Mrisho Kikwete in conversation with the Minister for Natural Resources and Toursim Hon. Lazaro Nyalandu during the 10th  Africa Travel Association Annual Presidential Forum on Tourism held at New York University Kimmel Center.
 The Director Africa House and Economics Professor at the  New York University Yaw Nyariko presents souvenir gift to President Dr.Jakaya Mrisho Kikwete during the 10th  Annual Presidential Forum on Tourism held at New York University Kimmel Center in New York this morning. Center is the Minister for Tourism and Natural Resources Hon. Lazaro Nyalandu.
 President Dr.Jakaya Mrisho Kikwete in a group photo with panelists and coordinators of the ATA 10th Annual Presidential Forum on Tourism  held at at New York University Kimmel Center in United States of America this morning. From left Executive Director Africa Travel Association(ATA) Mr. Edward Bergman, Namibia’s Minister for Environment and Tourism Hon. Pohamba Shifeta,(second left), Kenya’s Cabinet Secretary in the Ministry of East African Affairs, Commerce and Tourism Hon. Phyllis Kandie(Third left),  Mali’s  Minister for Culture, Crafts and Tourism Hon. N’Diaye  Ramatoulaye Diallo(fourth left),The President, The Minister for Natural Resources and Tourism Hon. Lazaro Nyalandu, Director Africa House and Professor of Economics Dr. Yaw Nyarko(seventh left), ), Uganda’s Minister for Tourism Wildlife and Antiquities Hon.Dr. Maria Mutagamba,(eight left) and the panel moderator who is also the CBS News Travel Editor Mr. Peter Greenberg(photos by Freddy Maro)
-------------------------------------------------------------------
Rais Kikwete afafanua changamoto za utaalii wa Afrika
·         Asema habari hasi kuhusu Afrika zinavuruga utalii wa Afrika

·         Asisitiza Tanzania itaendelea kupambana na ujangili


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete ameelezea changamoto kubwa zinazozuia kukua haraka zaidi kwa sekta ya utalii katika Afrika na hivyo kuliwezesha Bara hilo kuchuma matunda makubwa zaidi kutokana na sekta hiyo.
Aidha, Rais Kikwete amesema kuwa pamoja na kuwa na vivutio vingi vya utalii, Bara la Afrika, bado linabakia nyuma kwa kiasi kikubwa katika kuvutia watalii wa kimataifa na katika mapato yanayotokana na utalii.
Rais Kikwete vile vile amesema kuwa Tanzania itaendelea kutenga eneo kubwa la ardhi yake kwa ajili ya hifadhi na pia itaendelea kukabiliana na ujangili dhidi ya tembo, ambao hata hivyo amesema kuwa umepungua katika mwaka uliopita.
Rais Kikwete ameyasema hayo leo, Alhamisi, Septemba 24 wakati alipotoa hotuba ya ufunguzi wa shughuli za Miaka 10 ya Chama cha Usafiri cha Afrika – Africa Travel Association (ATA) na Miaka 10 ya Jukwaa ya Rais Kuhusu Utalii – Presidential Forum on Tourism kwenye Kituo cha Kimmel cha Chuo Kikuu cha New York (New York University Kimmel Center) Africa House, mjini New York.
Rais Kikwete yuko New York, Marekani kwa ajili ya kuhudhuria shughuli za mwaka huu za Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa (UNGA) baada ya kumaliza kuendesha vikao vya Jopo la Watu Mashuhuri Duniani ambao wanatafuta jinsi gani dunia inavyoweza kujiandaa vizuri zaidi kukabiliana na magonjwa ya mlipuko ambavyo pia vilifanyika New York.
Rais Kikwete ametambulishwa na kukaribishwa kutoa hotuba yake na Dkt. Yaw Nyarko, Raia wa Ghana na Mkurugenzi wa Africa House ambaye pia ni Profesa wa Uchumi kwenye Chuo Kikuu cha New York na Bwana Edward Bergman, Mkurugenzi Mtendaji Mwanzilishi wa ATA.
Alikuwa ni Rais Kikwete na familia ya Bergman ya New York ambao walianzisha na kujadili wazo la  kuanzishwa kwa chama hicho miaka 10 iliyopita.
Kabla ya kutoa hotuba yake, washiriki wa Kumbukumbu hiyo ya miaka 10 wamesikia maelezo ya kina kutoka kwa mawaziri wa nchi tano za Afrika kuhusu hali ya utalii katika nchi hizo na katika Bara la Afrika kwa jumla.
Mawaziri waliozungumza kwenye shughuli hiyo iliyoendeshwa na Bwana Peter Greenberg, Mhariri wa Usafiri wa Televisheni ya CBS ni Mheshimiwa Lazaro Nyalandu wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Maria Mutagamba, Waziri wa Utalii, Wanyamapori na Nyaraka wa Uganda ambaye pia ni Rais wa ATA na Mheshimiwa N’Diaye Ramatoulaye Diallo, Waziri wa Utamaduni, Utalii na Usanii wa Vinyango wa Mali.
Mawaziri wengine ambazo wamezungumza katika shughuli hiyo ni Mheshimiwa Phylis Kandie ambaye ni Waziri wa Masuala ya Afrika Mashariki, Biashara na Utalii wa Kenya na Mheshimiwa Pohamba Shifeta, Waziri wa Mazingira na Utalii wa Jamhuri ya Namibia.
Akizungumza katika shughuli hiyo, Rais Kikwete amesema kuwa changamoto kuu zinazokabili maendeleo ya utalii katika Afrika ni miundombinu ya kitalii, utangazaji wa masoko ya utalii na matatizo ya usafiri wa anga kuingia na kutoka Afrika.”
“Lakini pia kuna jambo kubwa la mtazamo hasi kuhusu Afrika. Kwa kawaida, vyombo vya habari vya nje vinalielezea Bara la Afrika kama Bara hatari ambalo sifa zake kuu ni migogoro, magonjwa na matatizo yanayotokana na umasikini. Haya yote siyo ya kweli ni upotoshaji wa makusudi.”
Ameongeza Rais Kikwete: “Ukweli kuhusu Afrika lazima uelezwe kwa usahihi na sisi wenyewe. Picha inayojengwa kuwa tatizo katika nchi moja ni tatizo la Bara zima siyo ya kweli na lazima itafutwe namna ya kulisahihisha jambo hilo. Afrika ni Bara la nchi 54 na siyo nchi moja ya majimbo 54.”
Ameongeza: “Ni upotoshaji huu ambao ulisababisha watu kufuta safari za kitalii kwenda Afrika wakati ugonjwa wa Ebola ulipolipuka katika Guinea, Liberia na Sierra Leone. Lakini Zanzibar katika Tanzania ni safari ya saa tisa za ndege kutoka nchi hizo tatu za Afrika Magharibi. Kwa hakika nchi hizo tatu ziko karibu zaidi na Bara la Ulaya kuliko ilivyo Kenya. Hili ni tatizo kubwa ambalo lazima lisahihishwe haraka iwezekanavyo.”
Kuhusu mapato ya utalii, Rais Kikwete amesema: “Mwaka jana, Afrika ilipokea watalii wa kimataifa milioni 56 ambalo ni ongezeko la asilimia mbili tu ya watalii wote wa kimataifa waliotembelea maeneo mbali mbali ya dunia na asilimia tano ya watalii wote waliotembelea dunia mwaka jana.”
Kuhusu Tanzania, Rais Kikwete amesema kuwa Tanzania inaendelea kutenga asilimia 36 ya eneo lake lote kwa ajili ya shughuli za hifadhi.
“Tumefanya hivyo tokea uhuru wetu. Tutaendelea kufanya hivyo. Kama mnavyojua pia tumekuwa tunakabiliana na changamoto ya ujangili ambao ulitishia kumaliza idadi ya tembo wetu. Tumechukua hatua na kuendesha kampeni dhidi ya janga hili. Sasa tunaanza kuona matunda ya juhudi zetu. Mwaka 2012 walikuwa wanauawa tembo sita kwa mwezi. Katika mwaka mmoja uliopita, hajauawa tembo yoyote.”

Rais Kikwete pia ameshangiliwa sana wakati alipowaambia washiriki wa shughuli ya leo: “Napenda kuchukua nafasi hii, vile vile, kuwaageni marafiki zangu wote wa ATA kwa sababu hotuba hii ni yangu ya mwisho nikiwa Rais wa nchi yangu. Nitaondoka madarakani baada ya Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 25, mwaka huu, 2015 baada ya kuwa nimekamilisha vipindi viwili vya uongozi wangu kwa mujibu wa Katiba ya Tanzania.”

0 comments: