
Nahodha
wa timu ya taifa ya Ghana, Asamoah Gyan, amekanusha madai kuwa alimtoa
kafara yake ambaye pia alikuwa mwanamuziki mashuhuri nchini Ghana
Castro.
Gyan amesema tetesi hizo ni za kushangaza sana wala hazina msingi.
Mwanamuziki
huyo aliyekuwa anaiimba nyimbo za mtindo wa Afrobeats, ambaye jina lake
halisi ni Theophilus Tagoe, alitoweka pamoja na rafiki yake Janet
Bandu, mnamo mwezi Julai.
Wawili
hao walitoweka wakati walipokuwa wamekwenda likizo na Gyan ambaye
alikuwa mchezaji wa zamani wa Sunderland, katika mji wa Ada.
Madai
katika vyombo vya habari nchini Ghana yanasema kuwa kutoweka kwa rafiki
ya Gyan kumezua wasiwasi baadhi wakidai kuwa huenda alimtoa kafara
mwanamuziki huyo.
Castro na rafiki yake Bandu, walionekana kwa mara ya mwisho wakielekea baharini na baadaye iliarifiwa kuwa walizama.
Miili ya
wawili hao haikuwahi kupatikana na madai yaliendelea kusambazwa mwezi
huu wakati ambapo kakake Gyan, Baffour Gyan alidaiwa kuwa mmoja wa genge
la vijana waliowashambulia wandishi wa habari waliohoji maswali kuhusu
madai hayo.
Hata hivyo baadaye aliachiliwa na polisi waliokuwa wamemkata kwa lengo la kumfungulia mashitaka.Tetesi hizo zilimfanya Gyan kuitisha mkutano na wandishi wa habari kuzungumzia madai hayo.
Wakili
wake Kissi Agbyabeng alitoa taarifa akisema kuwa familia ya Gyan
imeshangazwa sana na madai hayo na iliamua kutosema chochote ili polisi
waendelee na uchunguzi wao.
Taarifa
hiyo ilisema: " Tumekuwa kimya huku madai na tetesi zikienezwa kila
upande katika vyombo vya habari. Tumekuwa kimya sio eti kwa sababu
tunaficha ukweli, bali kwa sababu hatuoni umuhimu wa kusema kilichojiri
mjini Ada. Tumekuwa kimya kwa sababu tunataka polisi wafanye kazi yao
bila kuingiliwa.''
0 comments:
Post a Comment