Kamanda wa Polisi Morogoro, Kaminshna Msaidizi wa Polisi (ACP) Leonard Paul akizungumza na wandishi wa habari.
Jambazi
mmoja akiwa na bunduki na risasi 47 pamoja na sare za jeshi la wananchi
ameuawa na wananchi weye hasira kali wakati akijaribu kukimbia baada ya
kufanya tukio la kuvunja duka na kuiba shilingi laki 7 katika eneo la
melela Mvomero mkoani Morogoro.
Kamanda
Polisi mkoa wa Morogoro Lenard Paul amemtaja mtuhumiwa amefahamika kwa
majina ya Antony Msandawe mkazi Kilosa Maghubike jambazi hilo usiku
lilifanya tukio la kuvunja duka ambapo alikua njiani kulekea kilosa
kufanya tukio jingine.
Hata
hivyo askari wa barabarani walimstukia ndipo wananchi wakasaidiana na
jeshi la polisi kumkimbiza ambapo alikamatwa na kupigwa na wananchi na
alifariki dunia akiwa njiani kueleka hospitali.
0 comments:
Post a Comment