Tuesday, October 14, 2014

Tuesday, October 14, 2014





























RAIS, Dk Jakaya Kikwete amesema wananchi hawawezi kupata ajira iwapo hapatakuwa na wawekezaji, hivyo halmashauri nchini likiwemo jiji la Mwanza, zitengeneze maeneo ya uwekezaji ili kukuza uchumi na ajira.

Dk Kikwete amedai watu wengi wanataa ajira lakini wawekezaji hawawataki. Uchumi hauwezi kukua kama maeneo ya kuwekeza kiuchumi hayatatengenezwa, watu watabaki kurundikana sehemu moja na kufukuzana na mgambo.
Dk Kikwete alisema hayo mwishoni mwa wiki, wakati akifungua rasmi jengo la Kitegauchumi la Hoteli ya Mfuko wa Pensheni wa PPF jijini hapa, lililojengwa kwa gharama ya sh Bilioni 12.03.
Huku akiifagilia PPF kwa kutumia vizuri pesa za umma, alisema faida kubwa ya uwekezaji ni kukuza uchumi na kutengeneza ajira, mfuko huo sasa unamshawishi aalike ma Rais wa nchi nyingine kuja kufanyia mikutano Mwanza, kwa kuwa Hoteli ya jengo hilo wanaweza kukaa.
“Watu wengi wanataka ajira lakini wawekezaji hawawataki, huwezi kupata ajira kama watu hawawezi kuwekeza. Moja ya majukumu ya PPF ni kuwekeza vitegauchumi ili mapato yawe mazuri na kulipa mafao bora kwa wanachama wake, hongereni sana,” alieleza Rais.
Alidai kipindi fulani alipokuja Meya wa jiji la Mwanza akiwa Leonard Bihondo, alimueleza kuwa halmashauri ya jiji lhilo ilikuwa imepima viwanja 3,000 lakini havikuwemo vya kuwekeza vitegauchumi hivyo sasa ni wakati muafaka wa halmashauri na jiji hilo kutengeneza maeneo mengi ya uwekezaji ili kukuza uchumi.
Rais Dkt Kikwete alililifagilia Jiji la Mwanza kwa utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo na uwekezaji mkubwa ambayo imeanza kubadilisha taswira ya Jiji  na mipango endelevu ya kutenga na kupima maeneo ya uwekezaji, makazi, biashara na viwanda hali ambayo italifanya kuwa kivutio na kituo cha mikutano na biashara kwa ukanda wa nchi za Maziwa Makuu barani Afrika. 
"Meya wa sasa ameeleza mipango ya Jiji nimeona ni mizuri sana vivyo Meya Stanslaus Mabula endelea na nigelipata kuwa na Mamea wengine kumi kama wewe hapa nchini nchi ingeshamili kwa maendeleo na kukua kiuchumi endelea, kaza moyo ili Jiji la Mwanza liendelee kustawi na kuwa Califonia ya Tanzania,"alisema
Awali Mkurugenzi mkuu wa PPF William Erio na Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya PPF Ramadhani Khijjah, walimueleza Rais kuwa mradi huo ni mojawapo ya shughuli za uwekezaji wanazozifanya kwa madhumuni ya kulinda thamani ya fedha za wanachama wao ili wawalipe mafao bora wakati wakistaafu.
Hadi Juni 30 mwaka huu mfuko ulikuwa umewekeza jumla ya sh 1.5 trilioni, katika maeneo mbalimbali nchini, umekusanya kiasi cha sh Bilioni 136.6 kama mapato yatokanayo na uwekezaji na kuvuka lengo la zaidi ya sh bilioni 93.99. “Uwekezaji huu unazingati mwongozo wa  uwekezaji uliotolewa kwa pamoja na Benki Kuu ya Tanzania (BOT), Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Sekta ya Hifadhi za Jamii (SSRA),” alieleza Kijjah na kuongeza kuwa mfuko huo umekua kutoka sh B 264 wakati Rais Kikwete akiingi amadarakani hadi kufikia sh Trilion 1.686 ukuaji ambao ni zaidi ya mara tano.
Alisema jengo la hoteli hiyo ya kisasa pamoja na kutoa ajira nyingi, lina vyumba 82 vya kulala wageni, sehemu za kupumzikia, kumbi tatu za mikutano ukiwemo unaoweza kuchukua watu 500, mgahawa wa kisasa na mfuko unapata mapato ya pango la Hoteli kiasi cha sh milioni 88.5 kwa mwezi sawa na sh B 1.06 kwa mwaka.


0 comments: