Monday, October 20, 2014

Monday, October 20, 2014

Mkuu wa wilaya, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kyerwa mkoani Kagera na mwaandishi wa habari mwandamizi wa ITV Bw.Cosmas Makongo wametishiwa maisha kuuwawa na kundi la wafanyabiashara ili wasiendelee kufuatilia biashara haramu ya kahawa katika maeneo ya mipaka ya nchi kwenda nchi jirani ya Uganda hali inayoikosesha serikali mapato na kuendelea kumdidimizi mkulima asiendelee kiuchumi.

Hayo yamebainishwa na Mkuu wa Wilaya ya Kyerwa Kanali mstaafu Benedicti Kitenga wakati akizungumza na ITV katika mahojiano maaLum ya kipindi cha ripoti maalum.Amesema kuwa baada ya serikali ya wilaya kwa kushirikiana na halmashauri kuanzisha doria ya kudhibiti biashara haramu ya magendo ya kahawa ikivushwa kwenda nchi jirani ya Uganda kupitia mto Kagera kumeibuka wimbi la wafanyabiashara wakitishia maisha ya watendaji wa serikali na kuhalibu gari la mwandishi wa habari ikiwa ni mbinu ya kukwamisha juhudi za kuwadhibiti. Akizungumzia sakata hilo mkuu wa mkoa wa Kagera Kanali mstaafu Fabiani Massawe amesema kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa itashughulikia swala hilo ikiwa ni pamoja na kuimalisha ulinzi na kuwaonya wanaojihusisha na biashara haramu ya kahawa waache mara moja vinginevyo watakamatwa na kufikishwa kwenye vyombo vya kisheria.

CHANZO: ITV

0 comments: