Monday, October 20, 2014

Monday, October 20, 2014

Ziara ya mwenyekiti wa Baraza la Wanawake wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema Halima Mdee imepata mapokezi makubwa jijini Mwanza ambapo amewataka wananchi wa jiji la Mwanza wasikubali kulazimishwa kuikubali katiba inayopendekezwa kwani haikuzingatia maoni ya wanachi ya kutaka uwazi katika rasilimali za nchi zilizopo zitumike kunufaisha wananchi badala yake katiba hiyo inawapa mamlaka vigogo kuendelea kunufaika na rasilmali za taifa huku wananchi wakiendelea kuumia.

Mdee ameyasema hayo wakati akizungumza na wananchi kwenye mkutano wa hadhara katika uwanja wa Frahisha jijini Mwanza ambapo amesema Chadema hawatakubali kupigia kura ya ndiyo rasimu ya  katiba inayopendekezwa kwani wananchi wakipendekeza katiba mpya  iweke wazi mikataba inagusa maslahi ya wananchi kwa kuhakikisha mikataba anayoingia rais inakuwa wazi katika magazeti ya serikali ili wananchi wajue watakavyonufaika na mikataba hiyo lakini katiba inayopendekezwa imetupilia mbali maoni hayo ambapo amesema  katika hiyo imejaa mapendekezo ya kulinda maslahi ya wachache na sio  wananchi masikini walio wengi.  Naye naibu katibu Bawacha taifa Kunti Yusuph na katibu wa vijana taifa Edward Simbeye wamewataka wananchi wa jiji la Mwanza kutokubali kuburuzwa kuipigia kura ya ndiyo rasimu ya katiba inayopendekezwa na badala yake waisome kwa umakini na wahakikishe wanachagua viongozi wanaofaa katika uchaguzi wa serikali za mitaa huku vijana wakitakiwa kuacha kushabikia watu wanaowalazimisha watanzania kupiga kura ya ndiyo katika rasimu inayopendekezwa. 

0 comments: