Alan Henning kushoto mda mchache tu kabla ya kukatwa kichwa na mtu aliyesimama kando yake.
Kundi la wanamgambo wa kiislamu la Islamic state limetoa ukanda wa
video unaoonyesha mateka Alan Henning raia wa Uingereza akikatwa kichwa.
Henning
mwenye umri wa miaka 47 ambaye ni dereva wa texi kutoka kaskazini mwa
Uingereza alitekwa nyara mwezi Disemba mwaka uliopita alipokuwa
akilifanyia kazi shirika moja la kutoa huduma za misaada kwa wakimbizi
nchini Syria.
Kundi la Islamic State ambalo limechukua udhibiti
kwenye maeneo ya mpaka kati ya Syria na Iraq tayari lishawaua waandishi
wa habari raia wa Marekani James Foley na Steven Sotlof pamoja na
mfanyikazi wa kutoa huduma za misaada kutoka Scotland David Haines.
Mapema
babake John Cantlie raia wa Uingereza ambaye anashikiliwa mateka na
wanamgambo wa Islamic State aliomba kuachiliwa kwa mwanawe.
CHANZO: BBC
0 comments:
Post a Comment