Rais wa FIFA Sepp Blatter
Mjumbe
wa zamani wa shirikisho la soka duniani amesema kuwa heshima ya Fifa
haitaweza kurudi mpaka pale Rais wa shirikisho hilo Sepp Blatter
atakapoachia ngazi.
Michael Hershman ameiambia BBC kuwa Sepp Blatter hanabudi kuondoka na kupisha mtu mwingine kukiongoza chombo hicho.
Amedai
kuwa hivi sasa yanatakiwa mabadiliko ya uongozi baada ya Fifa kuwa
katika mlolongo wa shutuma za rushwa kwa miaka mingi,hivyo basi ni vyema
uongozi ukabadilika.
Blatter amekuwa Rais wa shirikisho hilo
tangu mwaka 1998 na mwezi uliopita alitangaza nia ya kuwania tena nafasi
hiyo ingawa aliahidi kuwa awamu ya nne ambayo ni sasa, ni ya mwisho.
Hershman
amesema anasikitishwa mno na hatua ya wadau wa nje hasa wadhamini
kutoingilia kati na kuchukua hatua stahiki, badala yake wamekuwa wakitoa
taarifa kwa vyombo vya habari wakisema wanatarajia kuona FIFA
ikitekeleza majukumu yake kwa kufuata maadili.
CHANZO: BBC
0 comments:
Post a Comment