Tuesday, November 4, 2014

Tuesday, November 04, 2014

Spika wa Bunge Mhe. Anne Makinda akisoma hotuba yake ya shukrani kwa wajumbe wa Mkutano wa 36 wa Bunge la SADC ambao ni Maspika na Wabunge kutoka Mabunge ya nchi wanachama wa SADC baada ya kuchaguliwa kuwa Rais wa Bunge hilo kwa miaka miwili ijayo Mjini Victoria Falls, Zimbabwe.<--!more-->Spika wa Bunge Mhe. Anne Makinda akielekezwa jambo na Katibu Mkuu wa Bunge la SADC Dkt. Esau Chiviya mara baada ya kukalia kiti cha Urais wa Bunge hilo baada ya kuchaguliwa rasmi kuwa rais wa Bunge hilo.Spika wa Bunge Mhe. Anne Makinda ambaye pia ni rais wa Bunge la SADC akiahirisha rasmi Mkutano wa 36 wa Bunge hilo baada ya Kumalizika jana. Makinda alichaguliwa kuwa Rais wa Bunge hilo na wajumbe wote wa Mkutano huo jana.
Spika wa Bunge la Zimbabwe Mhe. Jacob Mudenda akimpongeza Spika wa Bunge Mhe. Anne Makinda baada ya kuchaguliwa kuwa rais wa Bunge la SADC kwa miaka miwili ijayo. Pembeni kulia ni Spika wa Bunge la Afrika Kusini Mhe. Baleka Mbete
Balozi wa Tanzania nchini Zimbabwe akimpongeza Makamu wa Rais wa Bunge la SADC Mhe. Njovya Lema (Malawi) baada ya kuchaguliwa katika nafasi hiyo sambamba na Rais wa Bunge hilo Mhe. Anne Makinda (katikati) jana wakati wa Kumalizika kwa Mkutano wa 36 wa Bunge hilo.


Hatimaye wajumbe wa Mkutano wa 36 wa Bunge la SADC ambalo linaloundwa na mabunge ya  nchi wanachama wa SADC (SADC PF) wamemchagua kwa kishindo Spika wa Bunge la   Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Anne Makinda kuwa Rais wa Bunge hilo kwa kipindi cha miaka miwili ijayo.Makinda ambaye alikuwa hana mpinzani katika uchaguzi huo, aliungwa mkono na wajumbe wote wa Mkutano huo ambao ni Maspika na Wabunge kutoka mabunge ya Nchi wanachama wa SADC jana tarehe 2 Novemba, 2014 wakati wa kuhitimisha Mkutano wa 36 wa Jukwaa la Mabunge ya SADC uliokuwa ukifanyika katika Hotel ya Elphant Hii iliyopo Mjini Victoria Falls Nchini zimbabwe.Msimamizi wa uchaguzi ambaye ni Katibu Mkuu wa Bunge la SADC Dkt. Esau Chiviya alisema kwa mujibu wa kanuni za uchaguzi za Bunge hilo, kanuni ya Kanuni ya 42 (2) i  inatamka wazi kuwa endapo kutakuwa na mgombea mmoja pekee, basi  atawahoji wajumbe na endapo watamkubali basi atamtangaza rasmi kuwa amechaguliwa kushika nafasi hiyo.“ Kwa kuwa Spika wa Bunge la Tanzania Mhe. Anne Makinda hana mpinzani na kwa kuwa nimewahoji na wote mmemuunga mkono, basi natangaza kuwa ndiye Rais mpya wa Bunge la SADC kwa miaka miwili ijayo”. Alitangaza Dkt. ChiviyaAwali kwa mujibu wa utaratibu wa uongozi ndani ya chombo hicho, Makinda alitakiwa kugombea nafasi hiyo pamoja na Spika wa Ushelisheli na Msumbiji ambao wote kwa pamoja hawakushiriki uchaguzi huo na kuamua kumuunga mkono Spika MakindaAkisoma hotuba yake ya shukrani kwa wajumbe wa Mkutano huo, Mhe. Makinda amewashukuru wajumbe wote walioshiriki katika uchaguzi na kumuunga mkono ili aweze kuwaongoza katika kipindi kingine cha miaka miwili.“ Ninalo deni kubwa kwenu kwa jinsi mlivyoniunga mkono na kama mnavyojua jukumu letu kubwa mbele yetu ni kuwa na Bunge imara la SADC jambo ambalo nawahakikishia kwa pamoja tutafanikiwaMakinda alisema kama mnavyojua, malengo makuu ya SADC PF ni kuwa na Bunge la kikanda litakalowakilisha mawazo ya pamoja kutoka kila Bunge la Nchi wananchama wa SADC, hili ndilo lengo kuuu la waasisi wa umoja huu walilokusudia wakati wa kuanzisha chombo hiki mwaka 1997 hivyo nasisi lazima tulienzi na kulitekeleza.Mhe. Makinda amesisitiza kuwa kwa miaka 17 iliyopita ya uhai wa Bunge hili la SADC wamefanikiwa kwa kiwango kikubwa kutimiza malengo yake kama ilivyojiwekea katika Katiba yake ambayo ni kukuza na kuimarisha utawala wa kisheria, Kusimamia Masuala ya usawa wa Kijinsia, Utawala bora,pamoja na kukuza demokrasia katika ukanda wa SADC.Aidha aliwakumbusha wajumbe na wanachama wa Bunge hilo kuwa, anachukua nafasi hiyo huku Bunge hilo likikabiliwa na changamoto lukuki za kiutendaji ambazo nyingine ni za kimuundo, kiuchumi na za kimkakati.“Bado kuna haja ya kutatua changamoto mbalimbali ndani ya Bunge letu hususani Ukosefu wa namna bora ya kuwasilisha maamumizi ya Bunge hili ndani ya Utaratibu wa Jumuiya ya Wanacham wa nchi za SADC, Uwajibikaji hafifu kuhusu maamuzi ya Bunge hili kwa nchi wanachama, ukosefu wa namna bora ya kushirikiana na Bunge la Afrika, mawasiliano hafifu kati ya Chombo hiki na Mabunge ya Nchi wananchama, Uhaba wa rasilimali watu na fedha za kuendeshea chombo hiki. Alisema MakindaMkutano wa huo wa Bunge la SADC umemalizika rasmi jana baada ya pia kuchaguliwa makamu wa Rais wa Bunge hilo ambaye ni Mhe. Njovya Lema Mbunge kutoka  nchni Malawi.

0 comments: