Maelfu ya wakenya waliandamana kwenye mitaa ya jiji la Nairobi,kulalamikia manyanyaso na mashambulizi ya hadharani ambayo yamewakuta wanawake kadhaa kutokana na kuvaa nguo zinazochukiza jamii.
Shambulio la karibuni lilitokea mwisho wa wiki,ambapo msichana mmoja alivuliwa nguo na kubaki uchi kwenye kituo cha basi,na kundi la wanaume ambao walimtuhumu kwa "kuwajaribu".Tukio hilo lilirekodiwa kwenye video na kurushwa kwenye mitandao kadhaa ya kijamii,hali iliyopelekea kupokewa kwa hisia kali na makundi kadhaa yanayotetea haki za wanawake na mwisho wake kupelekea maandamano.
"Kama wanawake wa kiafrika,tunafundishwa namna ya kukaa kimya," anasema Caroline Chege,ambaye alishiriki kwenye maandamano, "lakini leo, tunaseema 'imetosha'"
Chege anasema hakujawa na usawa jinsi ambavyo jamii inauchukulia uvaaji wa wanaume na wanawake jijini Nairobi."Wanaume wanatembea hadharani wakiwa wamevaa kaptura tena bila mavazi mengine yoyote lakini hakuna anayesema kitu,"anaendelea... "Lakini mwanamke akivaa kwa namna fullani isyowaridhisha wanaume,watamvua nguo na kukiuka haki zake za msingi za kibinadamu."
Mamlaka zimesema zinayachunguza matukio lakini hakuna hata mtu aliyekwisha kamatwa.Chege anaitaka serikali ihusike kikakamilifu, na anachukizwa na ukimya wa rais Uhuru Kenyatta juu ya jambo hili.
"Rais ana binti ambaye bado ni mdogo,na pia ana mke",Chege anaeleza "nahitaji rais azungumze kwa ajili ya wanawake."
Waandamanaji wametaka uwepo mfumo wa kumbukumbu utakaoorodhesha majina ya watu ambao wamehusika kufanya mashambulizi ya kijinsia dhidi ya watoto na wanawake. "Polisi wanasema hawajawajua wahusika wa hayo mashambulizi," Chege anasema, lakini kwa shambulizi hili linaloonekana kwenye video polisi wangeshituka na kuchukua hatua zinazokubalika.
0 comments:
Post a Comment