Monday, November 10, 2014

Monday, November 10, 2014

Mombasa


Waandamanaji walipora maduka na kuwarushia mawe polisi kupinga kupigwa risasi na kuuwawa kwa mtu anayeshukiwa kuwa mpiganaji Muislamu.
Polisi wanakanusha kuwa walihusiuka na mauaji hayo yaliyotokea Jumamosi ya Hassan Guti, ambaye alihusishwa na mauaji ya afisa mwandamizi wa polisi mwezi Agosti.
Inaarifiwa kuwa ghasia zilizuka Jumapili baada ya mazishi ya Bwana Guti.
Watu kadha wa msimamo mkali wa kidini wameuwawa mjini Mombasa katika miezi ya karibuni.
Kumetokea mashambulio kadha ya mabomu mjini humo, ambayo yanashukiwa kufanywa na kundi la wapiganaji Waislamu wa Somalia, Al Shabaab.

0 comments: