Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amefanya uteuzi
wa Makatibu Wakuu wa Wizara kwa kuteua Makatibu Wakuu wanne wapya na
kuhamisha mmoja. Aidha, Rais Kikwete amefanya uteuzi na uhamisho wa Makatibu Tawala wa Mikoa.Taarifa iliyotolewa mjini Dodoma jioni ya leo, Jumatano, Novemba
5, 2014 na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue imesema kuwa
walioteuliwa kuwa Makatibu Wakuu ni Dkt. Donan Mmbando ambaye anakuwa
Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Dkt. Yohana Budeba
ambaye anakuwa Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi,
Mhandisi Mbogo Futakamba kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji na Dkt.
Adelhelm James Meru ambaye anakuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Utalii na
Maliasili.Kabla ya uteuzi wake, Dkt Mmbando alikuwa Mganga Mkuu wa
Serikali, Dkt. Budeba alikuwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Maendeleo
ya Uvuvi na Mifugo, Mhandisi Futakamba alikuwa Naibu Katibu Mkuu, Wizara
ya Maji na Dkt. Meru alikuwa Mkurugenzi Mkuu, Mamlaka ya Maeneo Maalum
ya Uwekezaji kwa Mauzo ya Nje (EPZA).Aidha, taarifa hiyo imesema kuwa Rais Kikwete amemhamisha Bibi
Maimuna Tarishi kutoka Wizara ya Maliasili na Utalii kwenda kuwa Katibu
Mkuu wa Wizara ya Katiba na SheriaKuhusu uteuzi na uhamisho wa Makatibu Tawala wa Mikoa, Rais
Kikwete amemteua Bw. Charles Pallangyo, Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya na
Ustawi wa Jamii kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Geita, Bw. Adoh Steven
Mapunda, Mkurugenzi Mtendaji, Manispaa ya Bukoba kuwa Katibu Tawala wa
Mkoa wa Arusha, Bw. Severine Kahitwa, Katibu Tawala wa Mkoa wa Geita
kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Kilimanjaro na Dkt. Faisal Issa, Katibu
Tawala wa Mkoa wa Kilimanjaro kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Mwanza.Wakati huo huo, Rais Kikwete amemteua Kanali (Mst) Joseph Simbakalia, Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, kuwa Mkurugenzi Mkuu wa EPZA.Uteuzi huo unaanza leo na Makatibu Wakuu na Makatibu Tawala wa
Mikoa wataapishwa kesho, Alhamisi, Novemba 6, 2014, Ikulu, Dar es
Salaam.Mwisho.Imetolewa na;Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,Ikulu – Dar es Salaam.05 Novemba,2014
0 comments:
Post a Comment