Katibu
Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Dkt. Florens Turuka akifungua Mkutano wa
Serikali na wadau wa Ukimwi kupitia utekelezaji wa programu za ukimwi
jana jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti
Mtendaji wa Tume ya Taifa ya kudhibiti Ukimwi (TACAIDS) Dkt. Fatma
Mrisho akizungumza na wadau mbalimbali walioshiriki Mkutano wa Serikali
na wadau wa Ukimwi kupitia utekelezaji wa programu za ukimwi jana jijini
Dar es Salaam.
Mwenyekiti
wa wadau wa Maendeleo kwenye sekta ya ukimwi Dkt. Michelle Roland
akiwasilisha mada wakati wa Mkutano wa Serikali na wadau wa Ukimwi
kupitia utekelezaji wa programu za ukimwi jana jijini Dar es Salaam.
Wadau
mbalimbali walioshiriki Mkutano wa Serikali na wadau wa Ukimwi kupitia
utekelezaji wa programu za ukimwi wakifuatilia kwa makini mada zilizokua
zikitolewa kuhusu kupunguza maambukizi ya ukimwi hadi kufikia sifuri.
Mwenyekiti
Mtendaji wa Tume ya Taifa ya kudhibiti Ukimwi (TACAIDS) Dkt. Fatma
Mrisho katikati akijadili jambo na mgeni rasmi Katibu Mkuu Ofisi ya
Waziri Mkuu Dkt. Florens Turuka kushoto. Kulia ni Mwenyekiti wa wadau wa
Maendeleo kwenye sekta ya ukimwi Dkt. Michelle Roland.
Katibu
Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Dkt. Florens Turuka aliyekaa katikati kwenye
picha ya pamoja na Wadau mbalimbali walioshiriki Mkutano wa Serikali na
wadau wa Ukimwi kupitia utekelezaji wa programu za ukimwi
Katibu
Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Dkt. Florens Turuka aliyekaa katikati kwenye
picha ya pamoja na Wadau mbalimbali walioshiriki Mkutano wa Serikali na
wadau wa Ukimwi kupitia utekelezaji wa programu za ukimwi. Picha na:
Genofeva Matemu - MaelezoSerikali kudhibiti ukimwi kifikia maambukizi
sifuri
Serikali
imepanga mikakati na kusimamia juhudi zinazofanywa na kuendelezwa na
wadau wa ukimwi kuhakikisha kuwa maambukizi mapya ya virusi vya ukimwi
yanapungua hadi kufikia sifuri ifikapo mwaka 2025.
Kauli
hiyo imetolewa na mwenyekiti mtendaji kutoka Tume ya kudhibiti Ukimwi
Tanzania (TACAIDS) Dkt. Fatma H. Mrisho wakati wa mkutano wa serikali na
wadau wa ukimwi kupitia utekelezaji wa programu za ukimwi jana jijini
Dar es Salaam.
Akizungumza
wakati wa mkutano huo Dkt. Mrisho amesema kuwa maambukizi ya ukimwi
yamepungua ukilinganisha na miaka 10 iliyopita kwani idadi imepungua
kutoka waathirika laki moja na elfu themanini hadi kufikia waathirika
elfu sabini na mbili kwa sasa.
Akitoa
mfano Dkt. Mrisho amesema kuwa Mkoa wa Njombe, Shinyanga, Dar es
Salaam, Mbeya na Rukwa ni mikoa ambayo inaonyesha kuwa na idadi kubwa ya
waathirika wa ukimwi hivyo kuwataka wadau wa ukimwi kutoka mikoa hiyo
kutoa elimu ya kutosha kwa jamii ili kupunguza maambukizi mapya ya
virusi vya ukimwi pamoja na magojwa ya zinaa.
Akifungua
mkutano huo, Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Dkt. Florens Turuka
amesema kuwa serikali imedhamiria kuanzisha mfuko utakaokua
unashughulikia masuala ya ukimwi wakati wa bajeti ya mwaka 2015/2016
wenye lengo la kuondoa maambukizi mapya ya ukimwi nchini.
Aidha
Dkt. Turuka ameitaka jamii kutowanyanyapaa waathirika wa ukimwi bali
wawapende na kuwapa moyo ili waendelee kuwa na afya bora kwani serikali
inawapigania na kuhakikisha kuwa wanatumia dawa za kuongeza maisha ili
kupunguza vifo vinavyotokana na ugonjwa huo.
Mkutano
wa serikali na wadau wa ukimwi kupitia utekelezaji wa programu za
ukimwi ulianzishwa mwaka 2003 ukifuatiwa na ule wa mwaka 2006 na
kuendelezwa kila baada ya miaka miwili ambapo mkutano wa mwaka huu ni wa
sita na umebeba kauli mbiu inayosema “Kwa yale mafanikio ambayo
tumeyapata mpaka sasa tunayaendeleza”.
0 comments:
Post a Comment