Thursday, November 20, 2014

Thursday, November 20, 2014
Rais wa Zimbabwe Robert Mugabe.
                                     Rais wa Zimbabwe Robert Mugabe.

Chama tawala cha Zimbabwe cha rais Robert Mugabe  ZANU PF, kinaendelea kukabiliwa na mvutano mkubwa na mgawanyiko wa kipekee wakati makundi mbali mbali ndani ya chama yanapigania ushawishi wa kisiasa kabla ya mkutano mkuu wa Disemba wa kuchagua viongozi wapya wa chama. Kundi linaloongozwa na makamu rais Joyce Mujuru na kile cha waziri wa sheria Emmerson Mnanganwa yanapingana kuchukua nafasi ya rais Mugabe atakapoacha madaraka.
Bw. Mugabe  ana umri wa miaka 90 hivi sasa.
Mkutano baraza la kisiasa ambalo bado linafuata mfumo wa kisiasa wa Urusi ya zamani unatarajiwa kufanyika siku ya  alhamisi kujadili mizozo hiyo ndani ya chama, hususan kuondolewa kwa maafisa wanne wenyekiti wa kamati mbali mbali ambao ni watiifu kwa makamu rais.
Viongozi zaidi kwenye mifumo ya majimbo waliodhaniwa kumuunga mkono Bi. Mujuru wanalengwa hasa baada ya rais Mugabe kuonekana kuegemea upande wa waziri wa sheria Mnangangwa, kufuatia kuingia mke wake kwenye siasa.
Bi Grace Mugabe amekuwa mstari wa mbele katika kutoa wito kwa  Bi Mujuru ajiuzulu, kutokana na tuhuma za kuhusika na ulaji rushwa na kutaka kumondoa  mume wake madarakani. Msemaji wa chama cha Zanu PF Rugare Gumbo anasema kuondolewa kwa wenyekiti hao wanne ni kinyume cha sheria.
Zaidi ya hayo mamia ya vijana wa ZANU PF wanaodaiwa wanamuunga mkono makamu rais kuanzia Jumatatu wameanza kukaa nje ya makao makuu ya chama huko Mutare  ili kulinda na kuzuia mipango ya kuletwa watu wengi wanaodaiwa ni wafuasi wa waziri wa sheria ili kuwasilisha malalamiko yao.

0 comments: