Friday, February 13, 2015

Friday, February 13, 2015
                  
                      Viongozi wa Ulaya katika mkutano wa kusitisha mapigano ya Ukraine. 

Viongozi wa mataifa ya Ulaya wamesema kuwa wataiwekea vikwazo zaidi Urusi iwapo itashindwa kusimamia makubaliano mapya yaliyofikiwa kusitisha mapigano Mashariki mwa Ukraine.
                                                 
Kansela wa Ujeruman Angela Merkel amesema kuwa tayari mataifa hayo yalishakubaliana vikwazo hivyo itakavyo wekewa Urusi iwapo itakiuka makubaliano hayo. Markel aliyasema hayo muda mfupi baada ya viongozi hao wa Ulaya kuwasilisha makubaliano yanayo zihusisha Ukaraine na Urusi kufuatia machafuko yanayoendelea. Usitishaji wa mapigano mashariki mwa Ukraine unatarajiwa kuanza rasmi Jumamosi usiku,hata hivyo wanajeshi wa Ukraine na Waasi wa Urusi wapo katika hali ya wasiwasi kufuatia makubaliano hayo mapya huku kila upande ukiangalia mwingine katika utekelezaji wa kuelekea kuleta Amani mashariki mwa Ukraine.

Chanzo: BBC

0 comments: