Mabingwa wa zamani na vinara wa sasa wa ligi kuu Vodacom, Yanga, wameendelea kujizatiti kileleni wakiwa Pointi 5 mbele ya timu ya pili na mabingwa watetezi, Azam FC, baada ya kuichapa Mbeya City magoli 3-1 kwenye mchezo uliopigwa leo hii kwenye uwanja wa sokoine jijini Mbeya.
Mabao ya Yanga hii leo yamefungwa na Simon Msuva, Mrisho Ngassa na Amisi Tambwe wakati lile la Mbeya City lilipachikwa na Peter Mapunda.
Katika mechi nyingine ya Ligi iliyochezwa Leo huko Shinyanga kwenye uwanja wa Kambarage, Stand United wameifunga Simba goli 1-0.
0 comments:
Post a Comment