Makamu wa rais Dk Mohamed Ghalib Bilall amesema Tanzania inaweza kufika malengo katika ujenzi endelevu kama wataalam wa ujenzi watafanya ujenzi wa majengo ya gharama nafuu yanayoenda sambamba na utunzaji wa mazingira kwa kuwashirikisha wataalam wa mipango miji ili kuwapunguzia wananchi ugumu wa maisha.
Makamu wa rais Dk Ghalib Bilall ametoa kauli hiyo katika mkutano wa wadau wa ujenzi wakiwemo wabinifu wa majengo kutoka baraza la ujenzi endelevu na mazingira Afrika Mashariki unaowashirikisha wataalam kutoka katika nchi za Afrika ya Mashariki.
Kwa upande wake rais wa chama cha wahandisi Tanzania Camilias Lekule amesema mazingira yanayo tumika katika kujenga majengo hapa nchini siyo rafiki kwa kuwa baadhi ya majengo yana haribu mazingira na hutumia nishati nyingi zenye gharama zisizo na ulazima.
Naye rais wa baraza la ujenzi endelevu wa mazingira mhandisi Ngwisa Mpemba amesema changamoto hizo zinaweza kutatuliwa kwa kufanya kazi kwa ushirikiano wa maafisa wa mipango miji ,diyo maana baraza limeamua kushirikiana nao kwa ukaribu huku Mkurugenzi Mkuu wa Shirika na Nyumba la Taifa Neemia Mchechu akidai kuwa shirika lake limefanikiwa kufanya ujenzi kwa utalaam wa juu na ndiyo shirika pekee ambalo limepata cheti maalum cha mafaniko ya ujenzi unaozingatia utunzaji wa mazingira.
0 comments:
Post a Comment