Friday, March 27, 2015

Friday, March 27, 2015
download

Kampuni ya ndege ya Fastjet ipo mbioni kutoa tiketi za bure kwa madaktari bingwa kwenda mikoani wanapoenda kuwapatia wananchi huduma za matibabu ili kuweza kupunguza gharama za nauli kwa wananchi kufika sehemu husika kupata matibabu,hiyo ikiwa ni hatua ya kurudisha kile kidogo wananchopata kwa jamii.
Hayo yamebainishwa na Meneja Mkuu Fastjet Afrika mashariki  Jimmy Kibati wakati wa kutambulisha safari zake mpya zitakazo anza mwishoni mwa mwezi huu ikiwa ni pamoja na kuzidi kupunguza bei kwa wateja wake wanaosafiri kwa ndege za shirika hilo.
Kibati alisema kuwa katika kuisaidia jamii wameshawasafirisha kwa kutoa tiketi bure kwa madaktari sita wa meno kwenda mkoani Shinyanga kutoa huduma na wakati wowote wapo mbioni mwishoni mwa mwezi kuwapeleka madaktari bingwa sehemu mbalimbali kuweza kutoa huduma ambazo wananchi wasiojiweza wangezifuata jijini Dar es salaam.
Alitanabaisha kuwa shirika hilo la ndege limekuwa na kawaida hiyo tokea lilipoanzishwa miaka miwili iliyopita,kutoa misaada kwa jamii isiyojiweza wakiwemo yatima na wajane kote nchini.
“Hapa tunatambulisha kuanza kwa safari za ndege zetu kutoka Kilimanjaro kwenda Mwanza,ambayo itakuwa kwa bei ya 35,000 na safari ya kutoka Kilimanjaro kwenda Entebe nchini Uganda kwa bei ya 95000  na safari hizi zitaanza mwishoni mwa mwezi huu”alisema Kibati.
Alisema kuwa watatoa safari tatu kwa wiki kuanzia Jumanne,Alhamisi na Jumamosi kwa kwenda Entebe na itafungua fursa kwa wafanyabishara pia safari ya Kilimanjaro na Mwanza itakuwa mara nne kwa wiki na kuwataka wananchi kusafiri kwa ndege hizo na kufurahia huduma zao.

0 comments: