Mtu mmoja amefariki dunia na kumi na mbili kujeruhiwa baada ya gari ya jeshi waliokuwa wamepanda huku ikiwa imebeba matofali kupinduka eneo la Mangamba nje kidogo ya mji wa Mtwara.
Akizungumza na waandishi wa habari baada ya kupokea majeruhi hao mganga wa zamu hodi namba nane katika hospitali ya mkoa wa Ligula Nora Kalinga amesema wamepokea majeruhi kumi na tatu na kati ya hao majeruhi aliyefahamika kwa jina la Shafii Mwaya amefia mapokezi kabla ya kupata matibabu kutokana na kuvuja damu nyingi.
Amesema hali za majeruhi wanne sio nzuri kutokana na kupondwa na matofali sehemu za kichwa, huku wengine hali zao zikiendelea vizuiri baada ya kutibiwa majeraha madogo madogo.
Baadhi ya majeruhi akizungumzia ajali hiyo amesema dereva alikuwa mwendo kasi na ghafla akawa anamkwepa dereva bodaboda eneo la kona na hatimaye gari kumshinda na kupinduka.
Hata hivyo mbunge wa jimbo la Mtwara mjini Hasnei Murji ambaye aliongozana na viongozi wa CCM wilaya ya Mtwara kuwajulia hali majeruhi hao amesema ameridhika na huduma iliyotolewa kwa majeruhi hao japo baadhi ya vijana hali zao sio nzuri.
Wengi wa vijana waliopata ajali ni wachezaji wa timu ya Buti moka kutoka naliendele ambao waliombwa kusaidia kubeba tofali hizo kutoka Mangamba na kuzishusha eneo la kambi ya jeshi naliendele nje kidogo ya mji wa Mtwara, ajali hiyo imetokea jana majira ya saa kumi na moja jioni hata hivyo kamanda wa polisi hakupatikana kutoa taarifa kamili juu ya ajali hiyo.
0 comments:
Post a Comment