Awali bungeni hapo kulijitokeza kutokuelewana kati ya wabunge wa vyama vya upinzani pamoja na spika wa bunge Mhe.Anna Makinda kuhusiana na muongozo wa mbunge wa Ubungo John Mnyika kuhusiana na uwepo au la kwa kura ya maoni ya katiba pendekezwa, kutokana na zoezi la uandikishaji wa wapiga kura kutokamilika kwa Mkoa wa Njombe wakati linatakiwa kukamilika kwa nchi nzima kabla au ifikapo Aprili 30 mwaka huu.
Katika miswada ambayo imewasilishwa na Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia Profesa Makame Mbarawa,inayohusiana na Sheria ya Miamala ya Kieletroniki na ule wa Sheria ya Makosa ya Mtandao wa mwaka yote ya mwaka 2015, Profesa Mbarawa amesema itasaidia katika kuona na kutatua mapungufu ambayo yamekuwepo awali kabla ya miswada hiyo kupelekwa bungeni.
Kama ilivyo ada Mwenyekiti wa kamati ya kudumu bunge ya miundombinu Peter Serukamba na msemaji wa kambi ya upinzani katika kamati hiyo kuhusiana na miswada hiyo Lucy Owenya, wametofautiana kuhusiana na umuhimu wa miswada hiyo kwa taifa.
Baadhi ya wabunge wamepongeza miswada hiyo na kusema kuwa imekuja kwa wakati muafaka.
Baadhi ya miswada ambayo imesomwa bungeni hapo kwa mara ya kwanza ni ule wa Sheria ya kupata habari, Sheria ya vyombo vya habari na ule wa marekebisho ya sheria ya ushindani,yote ikiwa ni ya mwaka 2015.
0 comments:
Post a Comment