Kwa mara ya kwanza baada ya kutoka kifungoni, bondia Francis Cheka (kushoto) akiwa jukwaani kupambana na bondia Kiatchai Singwancha, kutoka China. Pambano hilo lililopigwa kwenye ukumbi wa PTA jana usiku jijini Dar es Salaam liliishia raundi ya saba kwa Cheka kumpiga Mchina kwa KO.
Cheka akiendelea kushusha makonde mazito kwa Mchina,ambaye ni dhahiri alizidiwa muda wote,hata wakati alipojaibu kujihami kwa kurusha ngumi za kushitukiza.
Bondia Mchina akikuaa chini baada ya kushindwa kuhimili masumbwi ya Cheka.
Cheka akitangazwa mshindi mwisho wa raundi ya saba,baada ya mpinzani wake bondia kutoka China kuzidiwa na hatimaye kukubali kushindwa.
0 comments:
Post a Comment