Luis Figo amesema “soka
limepotea” baada ya Sepp Blatter kuchaguliwa tena kuwa rais wa Fifa jana
na kumtaka kwa mara nyingine tena kuondoka katika nafasi hiyo.
Blatter (79) alimshinda
mpinzani wake Prince Ali kutoka nchini Jordan, ambapo sasa atakaa tena
madrakani kwa miaka minne mingine huku akiwa amekaa madarakani kwa
takribani vipindi 5 vya miaka minne minne.
Blatter alipata kura 133 dhidi ya 73 za Prince Ali kabla ya mpinzani wake huyo kuamua kujitoa katika raundi ya pili.
Ushindi wake umekuja huku
viongozi 14 wa shirikisho hilo wakiwa wamekamatwa kwa tuhumu za rushwa
siku chache tu kabla ya uchaguzi huo kufanyika ambapo kulikuwa na mashinikizo kadhaa kwa kiongozi huyo kujiuzulu.
Figo, mwanasoka mkongwe wa Ureno ambaye awali
alipanga kuwania nafasi hiyo kabla ya kujitoa kwa madai ya kutozigawa
kura ili kurahisisha kumng’oa Blatter, amesema kuwa amehuzunishwa sana
na matokeo ya uchaguzi huo.
“Leo ilikuwa ni siku nyngine ya
giza hapa Zurich,” alisema nguli huyo wa Ureno. “Fifa imepotea, lakini
juu ya yote hayo, soka limepotea na kila mpenda soka amepotea pia.
“Blatter alitoa sababu za
kijinga sana pale aliposema hawezi kudhibiti kila mtu ndani ya
shirikisho. Hilo ni kama tusi kwa wapenda soka. Hawa watu, ambao Blatter
amekuwa akiwatunuku vyeo kwa miaka kadhaa, leo anawageuka, Fifa sio
shirikisho lenye maadili tena.
“Kama Blatter alihusika kwa
udogo katika soka, basi sidhani kama angechaguliwa. Kama ana upungufu wa
maadili, basi ndani ya miaka michache ijayo atajiuzulu.”
0 comments:
Post a Comment