Tuesday, June 23, 2015

Tuesday, June 23, 2015
 
Waziri wa maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu na balozi wa Marekani, Mark Childress wakisaini mktaba wa kulinda mazingira, Kukuza uhifadhi na Utalii nchini jana, Tarangire mkoani Arusha ambapo serikali ya Marekani imetoa dola milioni 14.5 na dola 2milioni kwa ajili ya vita dhidi ya ujangili(Sh20bilioni) kwa ajili ya mapambano dhidi ya ujangili

Serikali ya Marekani imetoa zaidi ya dola Bilioni 30 kwa ajili ya Kulinda mazingira na kukuza uhifadhi wa Utalii nchini. Makubaliano hayo yalishuhudiwa jana, Seronera mkoani Arusha kwa waziri wa Maliasili na Utalii Lazaro Nyalandu na Balozi wa Marekani nchini, Mark Childress kusaini makubaliano ya dola 2milioni kwa ajili ya kuendeleza mapambano ya ujangili, huku nyingine milioni 14.5 kwa ajili ya uhifadhi. 
 
 Katika hafla hiyo balozi wa Marekani Bw.Mark Childress, alimwelezea Nyalandu, kuwa ni mwanasiasa jasiri na makini asiyeogopa kusema ukweli hata kama unaumiza. Balozi Childress aliendelea kusema: waziri huyo ni tofauti na wanasiasa wengine na kwamba, ujasiri wake katika utendaji unapaswa kuungwa mkono. 
 
Kauli hiyo imetokana na hatua ya hivi karibuni ya Waziri Nyalandu kuweka hadharani idadi ya tembo waliopo nchini na kueleza bayana kuwa, tatizo hilo bado ni janga kwa taifa. 
 
“Kwa mwanasiasa mwingine ingekuwa ngumu kutoa taarifa kama ile kwani angeona anajimaliza lakini alilazimika kufanya hivyo ili njia za kutokomeza tatizo hilo ipatikane na sasa marafiki wa uhifadhi tumeamua tupambane pamoja kulaliza tatizo hili”. 
Pia, katika taarifa yake Nyalandu hakusita kueleza kutoweka kwa tembo 10,000 ambao hawakuweza kuonekana wakati wa sensa ya mwaka 2014 iliyofanywa na Taasisi ya Utafiti wa Wanyamapori (TAWIRI) kwa kushirikiana na mashirika ya kimataifa. 
Akizungumza wakati wa kutia saini makubaliano na uzinduzi wa mradi mkubwa wa kulinda mazingira, kukuza uhifadhi na utalii nchini wa PROJECT, ambapo serikali ya Marekani imetoa zaidi ya sh. Bilioni 31 katika utekelezaji wa mradi huo. 
 
Uzinduzi huo ulifanyika jana katika hoteli ya Treetops iliyopo ndani ya eneo la Hifadhi ya Wanyamapori inayosimamiwa na jamii (WMA) kwenye Hifadhi ya Taifa ya Tarangire. 

 
 Waziri wa maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu na balozi wa Marekani, Mark Childress wakioingezana baada ya  hati za mkataba wa kulinda mazingira, Kukuza uhifadhi na Utalii nchini jana, Tarangire mkoani Arusha ambapo serikali ya Marekani imetoa dola milioni 14.5 na dola 2milioni kwa ajili ya vita dhidi ya ujangili(Sh20bilioni) kwa ajili hiyo. mapambano dhidi ya ujangili
 
Waziri wa maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu na balozi wa Marekani, Mark Childress wakibadilishana hati za mkataba wa kulinda mazingira, Kukuza uhifadhi na Utalii nchini jana, Tarangire mkoani Arusha ambapo serikali ya Marekani imetoa dola milioni 14.5 na dola 2milioni kwa ajili ya vita dhidi ya ujangili(Sh20bilioni) kwa ajili hiyo. mapambano dhidi ya ujangili

0 comments: