Sunday, August 2, 2015

Sunday, August 02, 2015



Mamlaka ya usafirishaji nchini Ufaransa imesema inachunguza mabaki ya ndege yanayodaiwa kupatikana katika kisiwa cha Ufaransa cha RĂˆunion katika Bahari ya Hindi, ambapo mamlaka hizo zinayachunguza mabaki hayo ili kubaini kama ni ya ndege ya Malaysia ya MH370 iliyopotea bila kuwa na taarifa zozote.

Taarifa kutoka Marekani zinasema wachunguzi hao ambao wameona picha za mabaki hayo wana uhakika mkubwa kwamba ni ya ndege hiyo ya Malaysia aina ya Boing 777 ambapo mabaki hayo ni sehemu ya bawa la ndege hiyo iliyopotea.

Akizungumza mjini New York Marekani, Waziri wa Usafirishaji wa Malaysia Liow Tiong Lai amesema nchi yake imetuma wataalamu zaidi kuchunguza mabaki hayo yaliyopatikna katika bahari ya hindi.

Ndege ya shirika la Malaysia Airlines ilipotea tarehe 8 mwezi Machi mwaka 2014 ikiwa na abiria 239 ambapo abiria wote walipoteza maisha na ndege hiyo kutoonekana kabisa wala kujulikana chanzo cha ajali hiyo. 
Hii inakuwa mara ya kwanza kwa ugunduzi wa mabaki baada ya jitihada za kimataifa kutafuta masalia ya ndege hiyo kutozaa matunda hapo mwanzo.

0 comments: