Sunday, August 2, 2015

Sunday, August 02, 2015
Pilikapilika za maandalizi ya maonesho ya nane nane kitaifa mwaka huu zimepamba moto ambapo mgeni rasmi katika maonesho hayo yatakayofunguliwa Jumatatu Agosti 3, 2015 anatarajiwa kuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Mizengo Pinda. Maonesho ya mwaka huu yanaongozwa na kauli mbiu “Matokeo Mkubwa Sasa, Tuchague Viongozi Bora kwa Maendeleo ya Kilimo na Ufugaji.”



Mratibu wa Maonyesho ya Nane Nane kutoka Wilaya ya Newala Ado Kiwangu akizungumza na wageni waliotembelea bustani ya michungwa kuhusu namna bora ya kuzalisha machungwa  na matumizi ya mbolea ya samadi inayoipa michungwa virutubishi stahiki.


Mfugaji wa Sungura Ahmed Juma Ntava akiwalisha sungura wakati wa maandalizi ya maonyesho ya nane nane kitaifa yatakayofanyika Lindi.


Mmoja wa watumishi wa Jeshi la Magereza nchini akivuna kabichi iliyokomaa tayari kwa matumizi ya mboga.



Afande Majid Nyange kutoka Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), (kushoto) akieleza namna ya kutumia mazingira ya asili kutengeneza jokofu yenye gharama nafuu kwa kutumia mkaa, miti, sakafu na nailoni yeusi kwa ajili ya kusharabu mwanga.


Eneo la ndani ya jokofu lililotengenezwa kwa mkaa.









0 comments: