Mbunge wa Bukoba Mjini, Balozi Hamis Kagasheki (katikati) akiwa na Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe(kulia) pamoja na Katibu Mkuu wa Chadema, Dk.Wilbroad Slaa (kushoto) wakati wa kuaga mwili wa Mwandishi Edson Kamukara katika viwanja vya Leaders Club Jijini Dar es Salaam.
Mamia ya wananchi,waandishi pamoja na wadau wa habari nchini, leo wamejitokeza katika kuaga mwili wa aliyekuwa Mhariri wa Mawio na Mwanahalisi online,Edson Kamukara aliyefariki mwishoni wiki kutokana kulipukiwa na jiko la gesi nyumbani kwake jijini Dar Es Salaam, na anatarajiwa kuzikwa Juni 29 mkoani Kagera.
Wakizungumza wakati wa kuaga kwa aliyekuwa Mhariri wa Mawio na Mwanahalisi online ,Edson Kamukara wamesema ni pigo kwa tasnia ya habari kutokana na kuwa ujasiri na uthabiti wa kusimamia kitu anachoamini kwa kuzingatia maadili ya uandishi wa habari .
Akizungumza juu ya kifo chake,Mwenyekiti wa Taifa wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Freeman Mbowe amesema kifo cha Kamukara ni pigo kutokana na kuwa na msimamo wa bila kuyumbusha na bahasha.
“ Ni bora kuishi kwa kusimama kwa muda mrefu kuliko kuishi kwa kupiga magoti kwa muda mfupi hiyo ikiwa ni kuangalia kutumia kalamu kwa wanyonge bila maslahi ya wanasiasa”amesema Mbowe
Kwa upande wa Mwenyekiti wa Makampuni ya IPP,ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama cha wamiliki wa vyombo vya habari nchini, Bw.Reginald Mengi amesema Kamukara alikuwa jasiri katika kufanya mambo yake kwa kusimamia misingi ya habari na alikuwa hangalii fedha.
“Kamukara angekuwa anaangalia fedha basi angekuwa tajiri kwani alikuwa ni mtu wa kusimamia misingi ya habari kwa ajili ya wanyonge”alisema Mengi.
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe akizungumza na Katibu Mkuu wa Chama hicho,Dk.Wilbroad Slaa wakati wa kuaga Mwili wa Mwandishi Edson Kamukara katika viwanja vya Leaders Club Jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Makampuni ya IPP,Reginard Mengi akisalimiana na Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) ,Freeman Mbowe wakati wa kuaga mwili wa Mwandishi Edson Kamukara katika viwanja vya Leaders Club Jijini Dar es Salaam.
0 comments:
Post a Comment