Mwandishi wa habari na mtangazaji maarufu nchini Abdallah Idrissa Majura ameahidi kufanya mapinduzi ya michezo katika jimbo la Kawe ambao utakuwa ni mfano kwa maeneo mengine na taifa kwa ujumla.
Aliyasema hayo akizungumza na vyombo vya habari mara baada ya kurejesha fomu za kuomba kugombea ubunge jimbo la Kawe kupitia Chama cha Mapinduzi, amesema endapo atapendekezwa na CCM kisha kuchaguliwa kuwa mbunge wa jimbo hilo ataanza na michezo mitano ambayo ni soka, mpira wa kikapu, netiboli, wavu na mpira wa mikono.
"Mungu akinijaalia nikatimiza ndoto yangu ya miaka mingi nitaanza na michezo hii ambapo tutaunda timu moja yenye wachezaji mahiri katika kila mchezo na zote zitajulikana kwa jina moja tu kawe united"alisema mtangazaji huyo ambaye pia ni mwanamichezo maarufu.
Amesema anashangazwa kuona michezo kama mpira wa kikapu, netiboli, wavu na mpira wa mikono haipigi hatua wakati haina gharama kubwa za uendeshaji kulinganisha na soka ambayo licha ya kuhitaji fedha nyingi pia kuna ubabaishaji mkubwa kwani viongozi wengi wa mchezo huo hufanya wametawaliwa na nia ya kupata manufaa binafsi.
Amesema kwa sasa hawezi kuweka wazi mikakati atakayotumia kuiinua michezo hiyo kwakuwa wakati wa kampeni haujawadia.hata hivyo amesema ameamua kuanza na michache kwa sababu kipindi cha miaka mitano ni kidogo hivyo kama atabeba mzigo wa mambo mengi atashindwa kutimiza ahadi zake.
Mtangazaji huyo ambaye anamiliki kituo cha ABM FM RADIO cha mkoani Dodoma amesema dhaimira yake ya kuinua michezo ilianza tangu mwaka 2010 alipoanzisha kituo hicho ambacho kinaongoza nchini kwakuwa na vipindi vingi vya michezo kulinganisha na radio nyingine.ABM ina kipindi cha michezo kila baada ya saa moja.
Kuhusiana na changamoto ya viwanja, mtangazaji huyo ambaye ameweka rekodi ya kushinda tuzo za michezo za baraza la habari tanzania EJAT kwa miaka mitatu mfululizo huku mwandishi wake akishinda tuzo zilizopita amesema anao mkakati wa kuandaa uwanja mmoja ambao utatumia na timu zote za jimbo la kawe kwa ajili ya kufanyia mashindano.
"Kama nitapendekezwa na kisha kuchaguliwa kuwa mbunge wa Kawe nimekusudia kuwashirikisha viongozi wenzangu jimboni tuuzungushie maduka uwanja wa tegeta nyuki kisha tuuwekee majukwaa kama azam complex naamini utakuwa ni chanzo kizuri cha mapato ya jimbo na pia wanamichezo kuutumia.
Mgombea huyo amesema ameuchagua uwanja huo wa Tegeta nyuki kwakuwa ni mkubwa na pia ni rahisi kufikiwa na wanamichezo kutoka sehemu mbali mbali kwani mabasi ya dalala dala yanaanzia hapo kwenda maeneo ya Kariakoo na Ubungo.
Majura ambaye pia amewahi kushinda tuzo ya chama cha waandishi wa habari za michezo nchini TASWA 1997/98 zipo njia rahisi za kupata fedha za kujenga maduka ya kuzunguka uwanja huo pia kutengeneza majukwaa na kuahidi mbinu hizo kuziweka hadharani pindi kampeni zitakapoanza rasmi.
Mtangazaji huyo maarufu wa vipindi vya michezo ambaye amewahi kufanyakazi Redio Tanzania,Radio One/ITV na BBC licha ya kuwa na diploma ya uandishi wa habari kutoka chuo cha uandishi wa habari Tanzania TSJ pia anayo shahada ya kwanza ya sayansi ya jamii kutoka Chuo Kikuu Huria cha Tanzania.
0 comments:
Post a Comment