Sunday, July 12, 2015

Sunday, July 12, 2015
 
Mgombea Urais kwa tiketi ya CCM 2015 Dk. John Magufuli


Dkt. John Pombe Magufuli ndiye mgombea urais kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi baada ya kuibuka na kura 1204 sawa na asilimia 87.1% ya kura zote zilizopigwa na wajumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM, leo mjini Dodoma.Magufuli amewashinda Balozi Amina Ali Salum  na Dkt. Asha Rose Migiro, ambao wote kwa pamoja waliingia hatua ya tatu bora.

HISTORIA FUPI YA MAGUFULI

Dk. John Pombe Joseph Magufuli, alizaliwa Oktoba 29, 1959 Wilayani Chato – wakati huo ikiwa Mkoa wa Kagera (sasa Mkoa wa Geita).


Ana Shahada ya Uzamivu ya Kemia (2006 – 2009) kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.


Mwaka 1991 – 1994, alisoma Shahada ya Uzamili (Kemia) katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, na baadaye Chuo Kikuu cha Salford nchini Uingereza.


Mwaka 1985 – 1988, alisoma Shahada ya Kwanza ya Elimu katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam akichukua masomo ya Kemia na Hisabati.


Mwaka 1981 – 1982, alisoma Diploma katika Chuo cha Mkwawa akichukua masomo ya Kemia na Hisabati.


Mwaka 1979 – 1981, alipata elimu ya juu ya sekondari katika Shule ya Sekondari Mkwawa, Iringa.


Mwaka 1977 – 1978, alisoma elimu ya sekondari katika Shule ya Sekondari Lake, Mwanza.


Mwaka 1975 – 1977, alisoma Shule ya Msingi Katoke, Biharamulo mkoani Kagera.

Mwaka 1967 – 1974, alisoma Shule ya Msingi, Chato.


Mafunzo
Machi 1984 – Juni 1984 alihudhuria mafunzo ya Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), Mpwapwa mkoani Dodoma.


Januari 1984 – Machi 1984 alikuwa JKT Makuyuni, Arusha.
Julai 1983 – Desemba 1983 alikuwa JKT Makutupora, Dodoma.


Uzoefu wa kazi
Mwaka 2010 – hadi sasa: Waziri wa Ujenzi na Mbunge wa Chato.
Mwaka 2008 – 2010: Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Samaki; Mbunge wa Biharamulo Mashariki (Chato).


Mwaka 2005 – 2008: Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi; na Mbunge wa Biharamulo Mashariki (Chato)


Mwaka 2000 – 2005: Waziri wa Ujenzi, na Mbunge wa Biharamulo Mashariki.

Mwaka 1995 – 2000: Naibu Waziri wa Ujenzi; na Mbunge wa Biharamulo Mashariki.

Mwaka 1989 – 1995: Mkemia Chama cha Ushirika cha Nyanza Cooperative Union (Ltd.), Mwanza.


Mwaka 1982 – 1983: Mwalimu Shule ya Sekondari Sengerema (akifundisha masomo ya Kemia na Hisabati).

Dk. Magufuli amepata tuzo mbalimbali za ndani na nje ya nchi.
Ameshiriki na kuongoza mikutano mingi ya kitaifa na kimataifa.

Ameandika vitabu na majarida mbalimbali. Ameoa na ana watoto kadhaa.

0 comments: