Tuesday, July 7, 2015

Tuesday, July 07, 2015

Shirika la habari la serikali nchini China, limeripoti ongezeko la wanandoa wanaotengana kufuatia matumizi ya kupita kiasi ya mtandao wa facebook jambo ambalo limefanya wapenzi kutumia muda mwingi kwenye mtandao huo.
 
Ripoti hiyo imedai kuwa ndoa nyingi zinavunjika na kupelekea kupeana talaka kutokana na wachumba wanatumia muda wao mwingi wakiwa kwenye mtandao  huo na hivyo wanawatenga wapenzi wao ambao mwisho wake huchepuka na kuonja asali nje ya ndoa.
 
Kulingana na takwimu za serikali, idadi ya watu wanaotoa talaka imeongezeka maradufu katika kipindi cha miaka kumi iliyopita ambapo sababu zingine ni kuwepo kwa njia rahisi ya kutoa talaka.
 
Sambamba na hilo inadaiwa kuwa utoji wa talaka bandia ni moja ya mbinu ya wapenzi kupanga njama ya kutengana rasmi ili kuepuka malimbikizi ya kodi na kisha wanaoana tena.
 
Inadaiwa kuwa wanandoa pia hutumia talaka kama njia ya kuepuka masharti makali ya kuthibiti kuwepo kwa nafasi za kazi na pia nafasi za kupata masomo.

0 comments: