Baada ya kuiona risasi rais alitembea taratibu kwenda kuichukua kabla ya kumtupia mmoja wa walinzi wake.
Meja Chris Magezi, msemaji wa kikosi maalum cha kumlinda rais amesema risasi hiyo ilidondoshwa na mmoja wa walinzi wa rais bila kujua.
“Risasi hiyo ilikuwa kati ya walizopewa vijana wetu. Alikuwa akipakia risasi kwenye bunduki yake na ndipo risasi moja ikadondoka kwenye zulia kwa bahati mbaya", alisema Meja Magezi.
Alisema risasi ilidondoka mapema kabla rais hajafika eneo ambalo alikuwa anakutana na viongozi kutoka madhehebu mbalimbali.
Aliendelea kusema kwamba,baada ya mlinzi kugundua upungufu wa risasi alianza kuitafuta lakini rais Museveni akaingia ukumbini na alifanikiwa kuiona kabla ya walinzi wake kubaini mahali ilpokuwa imedondokea.
Washiriki kwenye mkutano huo walitazama kwa mshangao wakati rais Museveni akiokota risasi hiyo na kuwaonesha kabla ya kuwalaumu walinzi wake kwa uzembe.
“Tutachukua hatua za kinidhamu ili tukio hili lisijirudie tena.Hata hivyo, hakuna haja ya kuwa na shaka sana kwa sababu katika hali ya kawaida jambo hili laweza kutokea ukiwa kazini". Hii haimaanishi kuwa usalama wa rais ulitatizwa ama kujaribu kutatizwa na tukio hili kwenye mkutano.
0 comments:
Post a Comment