Wednesday, July 22, 2015

Wednesday, July 22, 2015


Aliyekuwa Mbunge wa Kahama kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi Mhe. James Lembeli (pichani) ametangaza rasmi kujivua uanachama wa Chama cha Mapinduzi CCM na kujiunga na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema).

Akizungumza na waandishi wa habari, Bwana Lembeli amelalamikia uongozi wa CCM Wilaya ya Kahama kwa kupandikiza chuki pamoja na kushindwa kuchukua hatua dhidi vitendo vya rushwa vinavyofanywa na baadhi ya wagombea vya kutoa shilingi elfu 5 kwa kila mwanachama wa CCM mwenyekadi siku chache kabla ya zoezi la kuchukua fomu za ubunge kuanza licha ya kutoa tahadhari na taarifa.

Aidha akizungumzia miaka tisa ya kufanya kazi katika nafasi ya ubunge wa jimbo la Kahama,Bwana Lembeli amempongeza rais Jakaya Kikwete kwa kurudisha jina lake kugombea nafasi hiyo katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2010 licha ya kuwa uongozi wa Wilaya ulishaliondoa katika orodha ya wagombea kutokana na mizengwe.

Katika hatua nyingine, mkurugenzi mtendaji wa hali halisi Publishers inayochapisha magazeti ya Mwanahalisi, Mseto na Mwanahalsi Online Bwana Saidi Kubenea amechukua fomu na kurudisha ya kuomba ridhaa ya chama cha Demokrasia na Maendeleo ya kugombea ubunge katika jimbo la Ubungo ili kusaidia kuleta mabadiliko kwa wananchi wa jimbo hilo pamoja kuongeza nguvu ya kutetea haki za wanyonge pamoja na uhuru wa vyombo vya habari.

0 comments: