Saturday, August 8, 2015

Saturday, August 08, 2015

Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani Mh. Pereira Ame Silima

Serikali imekiri kuwa wimbi la mauaji na uporaji wa silaha kwenye vituo mbalimbali vya polisi hapa nchini vinachangiwa na uzembe wa askari polisi, kutokuwa makini kazini, ulevi na kukaribisha watu wasiowajua undani wao wakiwa wamebeba silaha.

Kauli hiyo imetolewa na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani Mh. Pereira Ame Silima wakati akifunga mafunzo ya awali ya Jeshi la Uolisi na uhamiaji katika Chuo cha taaluma ya Polisi Moshi (MPA).

Amesema askari polisi wengi wanajisahau wawapo kazini na baadhi yao kulala. kutowatilia shaka watu wanaoingia katika vituo vya polisi ,kutofanya ukaguzi jambo ambalo linasababisha askari kuvamiwa na wahalifu kiholela.

Katika hatua nyingine,Naibu Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini Abrahaman Kaniki amepiga marufuku kwa askari wa jeshi la Polisi kujihusisha na ushabiki ama kuwa na itikadi za kisiasa na wagombea wakati huu wa kuelekea uchaguzi mkuu.

Baadhi ya viongozi wa dini waliotoa nasaha zao wamesema tatizo la rushwa na ukosefu wa maadili kwa watumishi wa uuma umesababisha wananchi wengi kukosa haki zao za msingi.

0 comments: