Wednesday, September 9, 2015

Wednesday, September 09, 2015

Raymond Richmond, Meneja wa kampuni ya Bia (TBL) Mwanza,akiwaonesha waandishi wa habari (hawapo pichani), mapumba ya mchele,yanayotumika kuzalisha nishati ya umeme wa kuendesha mitambo ya kiwanda hicho.Kulia ni Meneja wa Maji na Nishati wa kampuni hiyo.

Mwandishi wa habari, Daniel Mkate (kushoto) akiwauliza maswali, Meneja wa  Kampuni ya Bia (TBL) Mwanza, Raymond Richmond na Meneja wa Maji na Nishati wa kampuni hiyo, Sunday Kidolezi, kuhusu  changamoto ya upatikanaji wa mali ghafi hiyo na madhara yake katika kuzalisha nishati na athari za mazingira.

Meneja wa Maji na Nishati wa kiwanda cha Kampuni ya Bia (TBL) Mwanza, Sunday Kidolezi, akifafanua jambo kwa waandishi wa habari kuhudu mradi huo wa uzalishaji wa nishati ya umeme,unaotumika kuendesha mitambo ya kiwanda cha kampuni hiyo kwa kutumia mapumba ya mchele na mashudu ya pamba.Wa kwanza kushoto ni Meneja wa kiwanda cha kampuni hiyo,Raymond Richmond.

0 comments: