Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC),Jaji Mstaafu,Damian Lubuva akizungumza na makundi maalum (hawapo pichani) jinsi watashiriki upigaji wa kura Oktoba 25 kwenye mkutano uliofanyika leo Ukumbi wa New Afrika Hoteli jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Chama Shirikisho la Watu wenye Ulemavu Mkoa wa Pwani Adam Shaban akizungumza juu jinsi ushiriki katika upigaji kura Oktoba 25 katika mkutano uliotishwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) uliofanyika leo katika Hoteli ya New Afrika jijini Dar es Slaam.
Sehemu ya washiriki wa makundi maalum katika mkutano wa NEC juu ya ushiriki wa watu wenye ulemavu katika upigaji kura oktoba 25 uliofanyika leo Hoteli ya New Afrika jijini Dar es Salaam.
Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imesema vyama vya siasa vitangaze sera zao kwa wananchi na sio kuingilia masuala ya utawala wa tume hiyo.
Hayo ameyasema leo,Mwenyekiti wa tume hiyo,Jaji Mstaafu,Damian Lubuva wakati alipokutana na makundi maalum jinsi watavyoshiriki uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 25 mwaka huu,amesema tume inafanya kazi kwa mujibu wa sheria hivyo vyama vya siasa viachie tume ifanya kazi yake.
Lubuva amesema kuwa vyama vimekuwa vikishughulika na watu hivyo tume itavichukulia hatua za kisheria kutokana na kukiuka kwa maadili ya uchaguzi.
Amesema mabadiliko ya uteuzi baadhi ya watendaji NEC ni suala kawaida kutokana watu kujaza nafasi zilizoachwa wazi.
Lubuva amesema Tume haiko tayari kuingiliwa katika masuala yao ya kiutawala kutokana na kile kinachofanyika kiko katika sheria.
Amesema matokeo yatatolewa katika kila vituo na kwa mwaka watatumia siku tatu katika uchaguzi kwa matokeo yote.
Lubuva amesema wakati uchaguzi visionekane vikundi vyovyote katika eneo la kituo cha kupigia kura vikisubiri matokeo.
0 comments:
Post a Comment