Wananchi wa mkoa wa Kagera na viunga vyake wamemuomba mgombea wa kiti cha urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli (pichani kulia) kuimarisha bei ya zao la kahawa ili waweze kuinuka kiuchumi kutokana na zao hilo kuwa ndio tegemeo la kibiasahara kwa wakazi wa mjji huo.
Dk.Magufuli jana alifanya mikutano ya kampeni katika maeneo ya Muleba, Nshamba, Kamachumu, Kemondo, Bukoba vijijini na kumalizia Bukoba mjini amewaambia wakazi wa mkoa huo kuwa baada ya serikali ya awamu ya nne kuimarisha mtandao wa barabara kutoka Bukoba hadi Dar es Salaam na nchi jirani, awamu ya tano imejipanga kuimarisha usafiri katika ziwa Victoria ambapo meli mbili zitanunuliwa.
Katika hatua nyingine, wananchi hao wameelezea shauku yao ya kuona usafiri wa majini katika ziwa Victoria ukiboreshwa.
Dk.Magufuli jana alifanya mikutano ya kampeni katika maeneo ya Muleba, Nshamba, Kamachumu, Kemondo, Bukoba vijijini na kumalizia Bukoba mjini amewaambia wakazi wa mkoa huo kuwa baada ya serikali ya awamu ya nne kuimarisha mtandao wa barabara kutoka Bukoba hadi Dar es Salaam na nchi jirani, awamu ya tano imejipanga kuimarisha usafiri katika ziwa Victoria ambapo meli mbili zitanunuliwa.
Kuhusu kuimarisha bei ya zao la Kahawa , Dk. Magufuli ameelezea mikakati aliyo nayo kuimarisha bei ya zao hilo ili liendelee kuwa zao kuu la biasahara na kuwanufaisha wakazi wa mkoa wa Kagera.
Aidha Dk. Magufuli ameonesha kushangazwa na kauli zinazotolewa na waliokuwa viongozi waandamizi wa serikali kuwa serikali haijafanya lolote na kuongeza kuwa viongozi hao wanapaswa kuwaomba radhi watanzania.

0 comments:
Post a Comment