Mkurugenzi Mtendaji TPDC, Dkt. James Mataragio akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu uzinduzi wa miundombinu gesi asilia, Miundombinu hiyo inatarajiwa kuzinduliwa rasmi na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete katika eneo la Madimba Mkoani Mtwara tarehe 10 Oktoba 2015.
Sehemu ya Kiwanda cha kuchakata gesi asilia kilichopo eneo la Madimba Mkoani Mtwara, eneo ambalo uzinduzi rasmi unatarajia kufanyika tarehe 10 Oktoba 2015.
Sehemu ya Kiwanda cha kuchakata gesi asilia kilichopo eneo la Madimba Mkoani Mtwara, eneo ambalo uzinduzi rasmi unatarajia kufanyika tarehe 10 Oktoba 2015.
Serikali ya Tanzania, kupitia Wizara ya Nishati na Madini kwa kushirikiana Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania ilianza kuutekeleza Mradi wa Bomba la gesi asilia Kutoka Madimba Mkoani Mtwara na Songosongo mkoani Lindi mwaka 2013.
Mradi huo umegharimu Dola za Kimarekani bilioni 1.225 ambapo asiliamia 95% ni mkopo wa masharti nafuu kutoka Benki ya Exim ya (China) na asilimia 5% ni pesa za ndani. Hadi kufikia mwezi Agosti miundombinu ya mradi huo ilikuwa imekamilika.
0 comments:
Post a Comment