Sunday, September 28, 2014

Sunday, September 28, 2014

PFP KUWATAJIRISHA WANANCHI WENYE KIPATO CHA CHINI WILAYA 6 NCHINI KUPITIA PROGRAMU YA PANDA MITI KIBIASHARA





Mkurugenzi  mtendaji wa PFP Dr Maria Tham akizungumza na  wanahabari ofisini kwake 
Vitalu  vya miti  vilivyopandwa na  wananchi  Njombe 
Miche  ya  miti  ambayo mbegu yake  imetoka Zimbabwe  iliyotolewa na PFP kwa  shirika la TANWAT Njombe 

Meneja Mawasiliano wa Mradi, George Matiko  wa  PFP  akiwa katika bustani ya  miche  ya miti 
Mwanakikundi   cha wakulima  wa maparachichi Njombe akitunza  bustani yake 
Mratibu wa  wakulima wadogo wa  miti Bw  Erasto  akizungumza na  wanahabari 
Miche ya  kisasa ya matunda 


Watenda kazi wa PFP  wakimsikiliza mkurugenzi  wao 
Mkurugenzi wa PFP  akiendelea kutoa ufafanuzi wa mradi 
Afisa  habari wa PFP Bi Lilian akichukua taarifa  juu ni  wafanyakazi wenzake 
Wanakikundi   cha miti  Kifanya  wakiwajibika kujitafutia  utajiri  kwa kupanda miti 
Wanakikundi cha upandaji miti kibiashara Kifanya  wakiwa katika kitalu  chao
Moja ya kitalu cha kuotesha miche ya miti kilichopo katika kijiji cha Kifanya wilayani Njombe; kitalu hicho ni cha wakulima wanaounda umoja wa wapanda miti Kifanya
Meneja Mawasiliano wa Mradi, George Matiko akifafanua jambo kwa wanahabari; aliyeketi ni Mkurugenzi wa Programu hiyo, Dk Maria Tham
Dk Maria Tham katika mahojiano na wanahabari ndani ya ofisi zao zilizopo mjini Njombe
Mwenyekiti wa kikundi cha wapanda miti wa kijiji cha Kifanya akitoa ufafanuzi wa shughuli zinazofanywa na kikundi chao


WANYANCHI wenye kipato katika wilaya 6 za mkoa wa Njombe ,Iringa na Morogoro wanatarajia kunufaika kiuchumi kupitia programu maalum ya Panda Miti Kibiashara(PFP) ambayo imeanza na mpango huo kwa kasi kubwa .

PFP imeanzisha programu hiyo ili kuwaondoa katika hali ya umasikini na kuwawezesha kupata maisha bora zaidi kwa kuanzisha kilimo hicho cha miti badala ya ilivyosasa kwa wakulima wengi kutegemea mazao ya biashara pekee na pale soko linaposhindikana hali ya maisha kiuchumi huyumba zaidi.

Akizungumza na wanahabari ofisini kwake mkurugenzi mtendaji wa PFP Dk Maria Tham alisema kuwa wilaya zitakazonufaika na mradi huo ni ,Kilolo na Mufindi kwa mkoa wa Iringa na mkoa wa Njombe ni Ludewa , Makete, Njombe wakati mkoa wa Morogoro ni wilaya moja pekee ya Kilombelo .

Alisema biashara ya miti itaongezeka kwa kuzingatia kwamba ifikapo mwaka 2025 inatarajiwa mahitaji ya malighafi viwandani na kuni yataongezeka kutoka mita za ujazo milioni 1.5 hadi milioni 3.7.

Hata hivyo Dk Tham alisema lengo kuu la program hiyo iliyoanza Januari mwaka huu ni kuongeza kipato kwa wananchi vijijini kwa kuwapa elimu ya upandaji wa miti kitaalamu kwa kutumia mbegu bora na kuhudumia mashamba ipasavyo kwa kuzingatia mipango ya matumizi endelevu ya ardhi.

“ Wananchi wanapanda miti ila bado hawapandi kitaalam na wengi wao wanavuna miti michanga zaidi na hivyo kukosa faida "

Alisema kuwa lengo kuu la program ni kuona wananchi wanapanda miti kisasa hasa ukizingatia kuwa mikoa ya Nyanda za Juu Kusini ina udongo unaofaa kukuza miti, mvua za kutosha, ardhi ya kutosha na wakazi wake wanapenda kupanda miti japo utaalam bado .

Mkurugenzi huyo aliongeza kuwa kwa kupitia program hiyo mipango ya matumizi endelevu ya ardhi itatengenezwa huku wananchi wanaopanda miti wakihamasishwa kuunda vikundi vya wakulima wa miti kwa nia ya kufanikisha shughuli za upandaji miti.
Katika kipindi cha miaka minne kuanzia sasa wananchi katika wilaya hizo watahamasishwa kupanda miti katika eneo lenye ukubwa wa hekta 15,000.
“Huku wakihimizwa kuanzisha shughuli mbalimbali za kujiongezea kipato wakati wakisubiri miti yao ikue na kufikia umri unaofaa kuvunwa,” alisema.
Mratibu wa mtandao wa wakulima wapandaji miti ya matunda Njombe na Mufindi Erasto Ngole alisema kuwa toka PFP wamefika katika wilaya zao hali ya wakulima kujiunga na vikundi vya upandaji miti ya matunda na ile ya mbao na nguzo uimeongezeka zaidi 

0 comments: